Adui

Mara nyingi wakristo wanapozungumza kuhusu “maadui” wao wanazungumzia dhambi ndani ya miili yao (ndani ya asili yao ya kibinadamu) na majaribu na tamaa ambazo hutoka huko. Hawa ni maadui kwa kuwa hutujaribu tufanye mambo kinyume na mapenzi ya Mungu. Maadui hawa pia wanaweza kuwa nguvu za kiroho kama vile roho ya nyakati ambayo huenda kinyume na roho mtakatifu. Shetani, mwovu pia huitwa adui. Maadui wa kidunia wa Israeli katika agano la kale ni picha ya hawa maadui wa kiroho katika agano jipya. (Waefeso 6:12; 1petro 2:11; 1Petro 5:8)