Asili ya Mungu au asili ya kimungu, ni safi kabisa na haiwezi kujaribiwa na uovu. Tumeahidiwa kuwa asili ya kimungu inaweza kuwa sehemu yetu kwa kujisafisha kutoka kwenye ufisadi katika ulimwengu ambao hutokana na tamaa zetu ovu. Tunapoishinda ya mwili wetu wenye dhambi hatua kwa hatua tunaibadilisha na asili ya kimungu – Mungu anashiriki asili yake na sisi. Kwa maana mwitikio wetu wa asili katika hali tunazokutana nazo katika maisha tumeushinda, “matendo ya mwili” kama vile wivu, kiburi, chuki, na ubinafsi zimebadilishwa na “tunda la roho” (Wagalatia 5:19-23). Kwa maneno mengine, mwitikio wa upendo, unyenyekevu, utu wema, furaha, n.k. vinakua asili yetu. Hii ndiyo maana ya kusema asili ya kimungu huwa sehemu ya maisha yetu. Hii inaitwa utakaso. (2Petro 1:2-4; 1Yohana 3:2-3; Yakobo 1:113; wagalatia 5)