Damu ya Yesu

Hii mara nyingi haimanishi damu ya kimwili iliyomwagika pale alipo sulubiwa Kalivari, lakini ni taswira ama ishara ya “damu” ambayo ilimwagika wakati ambapo Yesu aliacha kufanya mapenzi yake na akaacha kuishi maisha yake.  Kwa kuziweka katika kifo dhambi katika mwili wake, katika asili yake ya kibinadamu, “damu” ilimwagika na hakuwa mwenye lawama, sadaka hii iliweza kutumika kulipa deni la dhambi zetu na kutupatia msamaha. Kwa akili ya kina, sisi kama sehemu ya mwili wake tumfuate, tunashinda dhambi ambazo zinaishi ndani yetu, na kwa wakati huo “damu” humwagika kutoka ndani yetu kama ishara ya kifo cha hizi dhambi. Kwa kuwa dhabihu isiyo na lawama, alisulubiwa kama mwenye dhambi japo kiukweli hakutenda kosa lolote, aliikubali adhabu ya dhambi na kifo chake (damu yake) ilitumika kama “malipo” kwa wale wanaomwamini, hivyo wanaweza samehewa dhambi zao na kusafishwa kutokana na dhambi zao za asili. (Mathayo 26:27-28; 1Wakorintho 11:25-26; 1Petro 1:18-19; Waebrania 10:19-22; Ufunuo wa Yohana 12:11; Waebrania 12:4; 1Yohana 1:7; Marko 10:45)