Dhiki

Dhiki au majaribu humaanisha matukio au hali ambayo hutaka kukufanya utende dhambi, ambazo husababisha mawazo ya dhambi na majaribu kuinuka ndani yako. Katika dhiki au majaribu mapenzi yako ya kumtumikia Mungu “hupambana” na tamaa ya kutenda dhambi. Dhiki au majaribu pia hujulikana kama nyakati ngumu ambazo hujaribu uwezo wako wa kusimama katika imani – katika kanisa la awali mara nyingi ilihusisha mateso kwa wakristo. (Warumi 5:3; Yakobo 1:2-3; 1 Petro 2:12-13)