Jitoe mwenyewe

Kujitoa mwenyewe, au kujitoa dhabihu mwenyewe, inamanisha kutumia kila kitu ulicho nacho kwa ajili ya kufanya mapenzi ya Mungu hapa duniani kuliko kufanya mapenzi yako. Hii inahusisha kuachana na maoni, hoja na hisia zote ambazo ziko kinyume na mapenzi ya Mungu, pamoja na kutoa muda wako, ujuzi wako, pesa zako, n.k. endapo Mungu atakuomba kufanya hivyo. (Yohana 15:13; Waefeso 5:2)