Kazi za mwili

“Kazi za mwili” au “matendo ya mwili” ni dhambi ya ufahamu, ni vitu ambavyo tunajua kwamba ni dhambi hata kabla hatujavifanya. Hizi siyo “ajali” lakini ni dhambi ambazo tunafanya tukijua. Tunahitajika kutubu kutokana na hizi dhambi na kuziacha mara moja tunapookolewa. “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.” Wagalatia 5:19-21.  (Wakolosai 3:5-9)