Kiti cha Neema

“Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.” Waebrania 4:16. Kwa kuwa yesu alijaribiwa lakini hakutenda dhambi, inawezekana sisi kuja mbele zake kwa ujasiri na kujiamini kupokea neema. Neema hii ndiyo itatusaidia pia tusitende dhambi tunapojaribiwa. Tunakuja katika kiti cha enzi cha Mungu katika maombi na hutusikia na kuona nia ya mioyo yetu. Hapo tunaunganishwa na nguvu ya mbinguni na nguvu hii inaweza kutusaidia kushinda dhambi zote.