Kuanguka dhambini ni sawa na kutenda dhambi. Ni pale unapojaribiwa kutenda dhambi nawe kwa kufahamu kabisa unakubali hayo majaribu au tamaa za akilini mwako, na unaruhusu tamaa hizi za dhambi, maneno, na matendo. Lakini ukianguka dhambini, maamuzi yako ya kumtumikia Mungu na kushinda dhambi hayabadiliki. Japokuwa umefanya makosa bado unahitaji kuishi huru toka dhambini. Kuanguka inahesabika kama “tukio la mara moja”. Kuishi katika dhambi kwa namna nyingine inamaanisha kwamba mtu hataki kuacha dhambi.
Neno “kuanguka” halipo katika biblia lakini inamanisha mwanzoni mwanadamu (Adamu na Eva) walipoiruhusu dhambi katika bustani ya Edeni. Kwa kufanya hivyo asili yao ya kibinadamu ikawa yenye dhambi, na hii imekua ikirithishwa kwa watoto wao na hadi kwa vizazi vyote vilivyokuja baada yao.(1 Yohana 2:1; Ufunuo wa Yohana 2:4-5)