kubadilishwa

Kubadilishwa ni kuchukua maamuzi ya kutoka dhambini na gizani, kutoka katika nguvu ya mwovu, na kuelekea kwa Mungu aliye hai. Tunatubu kutokana na dhambi zetu za zamani, kuacha njia zetu za zamani – ambapo tulifurahia kuishi katika dhambi – na tunapata akili mpya ambapo tunafanya maamuzi imara “kukataa” kutenda dhambi (Kuyakataa majaribu). Ni muhimu pia, baada ya kubadilishwa hatuendi tena katika maeneo ama kwa watu waliokua na ushawishi mbaya kwetu kabla hatujabadilishwa, la sivyo mambo yanaweza kwenda ovyo tena. (matendo ya mitume 3:19; Matendo ya mitume 26:18; Waefeso 4:22-24; 1Petro 2:1-2.)