Kuchukia maisha yako mwenyewe

Kuchukia maisha yako inamanisha kuchukia uchoyo, majivuno, ubinafsi, na asili ya dhambi inayoishi ndani yako. Unachukia sehemu ya mwili wako ambayo imefanywa kuwa fisadi na dhambi. Haina la kufanya dhidi ya hali kujithamini kwa hali ya chini (hali ya kujisikia vibaya juu yako mwenyewe) au kujihisi kuwa katika hali duni (hali ya kujihisi hauko vizuri kama wengine, kujihisi kama hauna thamani), hali ambayo haiji kutoka kwa Mungu. Kuchukia maisha yako (dhambi katika asili yako ya kibinadamu) ni moja kati ya vitu vinavyohitajika kuwa mwanafunzi wa Yesu. (Yohana 12:25; Luka 14:26; Warumi 7:15-18)