Kuzaliwa mara ya pili ni kitu ambacho huchukua nafasi kwenye maisha ya mkristo wa kweli. Unatupilia mbali aina ya maisha yako uliyokua ukiishi na kufikiria, ambapo ulikua ukiishi kwa kufuata mwili wako wenye dhambi unazaliwa mara ya pili katika maisha pamoja na kristo; unakua mpya wa kiroho na wa milele. “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! yamekuwa mapya.” 2Wakorintho 5:27. baada ya kuzaliwa mara ya pili unauona ufalme wa Mungu kama lengo lako kuu na kila jambo lisilohusiana na ufalme wa mbinguni linakua uchafu kwako. Soma kuhusu kuzaliwa katika roho kwa Paulo katika kitabu cha Wafilipi 3:4-10.