Linda moyo wako (akili yako, mtazamo wako, maisha yako ya ndani na uhusiano wako na Mungu) Ni sawa na kusafisha moyo wako. Ni pale unapohakikisha kwamba hakuna jaribu kwa namna yoyote ya uchafu au mawazo ya dhambi yatakayoruhusiwa kuingia ndani ya moyo wako, lakini yatazuiliwa yatakapokuwa katika hali ya mawazo. Ni kuwa makini dhidi ya ushawishi wa mwovu katika maisha yako ya kiroho. (Mithali 4:23)