Mapambano

Tunapozungumzia mapambano na vita katika maisha ya kikristo, huwa inamaanisha mapambano ndani yetu ambayo huchukua nafasi pale mawazo maovu yanapotujaribu tutende dhambi. Roho wa Mungu na mwili wetu wenye dhambi huwa katika mafarakano. Unapoamua kufanya mapenzi ya Mungu pekee na unaongozwa na roho, ndipo huwa na mgogoro kati ya mwili na roho: haya ndiyo mapambano ambapo unahitajika kushinda majaribu na kuishinda dhambi hiyo. (Wagalatia 5:16-17; Waebrania 12:4)