Matendo ya mwili

Matendo ya mwili (warumi 8:13) ni mambo ambayo tunagundua kuwa ni mabaya baada ya kuyafanya, kwa sababu roho mtakatifu hutufunulia; ndipo macho yetu hufunguliwa katika ukweli kwamba yalikua mambo mabaya. Kwa hivyo mambo yote tufanyayo bila kutambua ndiyo matendo ya mwili. Hatutiwi hatiani wala hatuadhibiwi kwa matendo haya ya mwili tunapokubali na roho anapotuonesha kwamba ni matendo mabaya, na ndipo tunayashinda kwa msaada wa roho mtakatifu. (Warumi 7:25; Warumi 8:1-2)