Mtu wa zamani

“Utu wako wa zamani” ni mawazo, njia yako ya kufikiria kabla haujakombolewa. Ni mawazo yanayoruhusu hamu na tamaa zako kutawala maisha yako; haujafanya maamuzi imara ya kupambana na dhambi. “Mtu mpya” ni mawazo yako baada ya kuokolewa. Ni maamuzi ya kuishinda dhambi na kuishi maisha ya haki na utakatifu. Ni akili ya kumtumikia mungu na mapenzi yake, kuliko mapenzi yako au tamaa kutoka mwili wako (asili ya binadamu yenye dhambi) utu wa zamani umevuliwa na utu upya umevaliwa, katika matendo ya imani, na ubatizo ndiyo ishara. (Warumi 6:1-6; waaefeso 4:22-24; Wakolosai 3:9-10)