Mwili wa kristo unaundwa na wale wote walioyatoa maisha yao kumtumikia Mungu na wanataka kuwa kama yesu. Hufanya kazi ambayo amewapa, ambayo huwa inatofautiana kati ya mtu na mtu, kwa kujijenga wenyewe na wengine na kutuunganisha sisi sote. Mwili wa kristo umeundwa na kila afanyae mapenzi ya Mungu hapa duniani kama inavyofanyika mbinguni, katika maisha yao na katika huduma ya Mungu na wengine. (Waefeso 4:11-16)