Mwili

“Mwili” ni tamaa ya dhambi/ majaribu/ hamu, n.k. ambayo huishi katika asili ya kibinadamu. Ni chanzo cha majaribu, na hakuna kilicho chema ndani ya mwili. (Wagalatia 5:19-21; Warumi 7:18; Wagalatia 5:24; Warumi 8:5) Katika tafsiri ya biblia zingine maneno kama “asili ya binadamu yenye dhambi”, “asili ya dhambi” n.k yanatumika badala ya “Mwili”

Dhambi ni kitu chochote ambacho kipo kinyume na mapenzi ya Mungu na sheria zake. Kutenda dhambi ni kuzidharau sheria hizi. Tamaa ya dhambi huishi katika asili ya kibinadamu. Kwa maneno mengine, asili ya mwanadamu imeundwa kwa ufisadi na imeshawishiwa vibaya na tabia na tamaa ya dhambi ambayo huishi ndani ya wanadamu kama matokeo ya kuanguka dhambini na kutotii katika bustani ya Edeni. Huu ni “mwili wa dhambi” (Warumi 6:6) tuliozaliwa nao. Biblia pia huziita hizi tabia na tamaa za dhambi “tamaa za mwili” au “hamu ya mwili”

Hii inamaanisha kuwa binadamu hujaribiwa na tamaa na mawazo yake mwenyewe yaliyo katika mwili wenye asili ya dhambi. Yohana aliandika sote “tuna dhambi” lakini hauna hatia kutenda dhambi labda utambue na kuzikubali tamaa hizi za dhambi. Dhambi inaweza “kuuawa” kidogo kidogo kwa kutozikubali hamu na tamaa kwa kuanza kuzichukulia kama dhambi. Hali hii mwanzoni ilitokea kwa Yesu alipokua kama mwanadamu hapa duniani. (1Yohana 1:8; Warumi 6:6; warumi 7:18; Warumi 8:3-4).

Neno “Mwili” linaweza pia maanisha mwanadamu au mwili wetu wakiumbo, hususani katika agano la kale. (Mwanzo 6:13; Zaburi 56:4; 1Petro 1:24; Waefeso 5:29)