Nguvu zangu mwenyewe

Hii hutumika mara nyingi mtu anapojaribu kuua tamaa zake za dhambi bila msaada wa Mungu; hujaribu kuacha dhambi kwa kutumia mapenzi yake yenye nguvu. Baadhi ya watu wanaweza fanikisha hili kwa kiasi fulani, lakini mwishoni huwa vigumu kuishinda dhambi moja kwa moja kwa kutumia nguvu yake mwenyewe – baada ya muda utafikia ukomo wa nguvu zao wenyewe, na mapenzi yao yenye nguvu. Mkristo anahitaji nguvu na msaada wa Roho mtakatifu kuishinda dhambi moja kwa moja. Sababu ya kawaida inayofanya watu kukata tamaa ni kwa sababu bado wanaamini katika nguvu zao wenyewe, na hawaweki tumaini lao lote kwa Mungu. (2Wakorintho 12:7-10; Zaburi 147:20-11; Zakaria 4:6)