Tembea katika nuru

Ukitembea katika nuru unaheshimu yote Mungu anayokuonesha kupitia roho mtakatifu. Mfano anakuonesha nia ya kushinda uvivu, au uongo au tamaa ya dhambi yoyote. Hii inamaanisha kuweka katika kifo kila dhambi unayooneshwa (kuangaziwa) na kuzitii amri zote Mungu anazokupa. Unapofanya hivi haubebi tamaa za mwili wako wenye asili ya dhambi. (1Yohana 1:7; Yohana 3:18-21; Yohana 8:12; Warumi 8:1-4; Wagalatia 5:16; Wagalatia 5:255)