Ushirika

Ushirika inaanisha hisia ya umoja na kushirikiana na wakristo wengine wanaoishi maisha sawa na unayoishi. Zaidi ya hapo ni kujengana kati ya mmoja na mwingine na kuwa na malengo sawa na roho ambayo huenda ndani zaidi kuliko urafiki na mahusiano ya kibinadamu. (1Yohana 1:7) Pia tunakuwa na ushirika pamoja na kristo tunaposhinda dhambi kama alivyofanya alipokua kama mwanadamu. Kwa njia hii tunapata kumjua na tunaweza kuwa na ushirika na umoja pamoja naye. (Wafilipi 3:10)