Je, maisha yako ni mfano wa ukweli?

Je, maisha yako ni mfano wa ukweli?

Watu wanapsawa kuona neno la Mungu kwenye maisha yetu.

23/11/20203 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Je, maisha yako ni mfano wa ukweli?

5 dak

“Basi Pilato akamwambia, wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi niezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye na hiyo kweli hunisikia sauti yangu.” Yohana 18:37.

Yesu ni kweli

Yesu alijua alichoitiwa kufanya. Hakuna ambaye angeweka kumyumbisha. Alijua ni kwa nini alikua amekuja na mahali alipokuwa anaenda. Alijua alichokua ameacha na kilichokuwa kinamsubiri alipozaliwa katika ulimwengu huu. Alikuwa amezaliwa kuushuhudia ukweli, kuwa mfano hai wa ukweli. Yesu ni kweli. Yeye ni njia, kweli na uzima.

Alikuwa mfalme wa kweli na haki. Aliishi na kutawala kwa ukweli. Hapa ulimwenguni alimkanyaga shetani, mwanamfalme wa uongo na giza, chini ya miguu yake. Kwa kuwa muda wote alikuwa mkweli na mwaminifu, alikuwa muwazi na hukumu kwa wote walioonana nae. Hii ndio sababu alichukiwa. Hakuwa na umbo la nje wala urembo (Isaya 53:2) ili watu wavutiwe nae. ( Isaya 53:2) aliwaambia wanafunzi wake, “ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi; bali hunichukia mimi; kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu.” Yohana 7:7

Yote unayopaswa kufanya ili upendwe na kila mtu ni kuenenda ukiwa na uso wenye tabasamu na kwa sifa; ndipo utakuwa na marafiki wengi. Lakini inagharimu kuwa mkweli na mwaminifu kila wakati. Kwa kweli, inagharimu kila kitu. Ndipo hautakuwa na marafiki wengi, lakini marafiki utakaokuwa nao watakuwa wenye thamani Zaidi. Watakuwa marafiki ambao hawatasema kitu kimoja wakimanisha kitu kingine tofauti. Watakuwa ambao unaweza kuwategemea kila wakati. Wanakuwa marafiki waaminifu ambao hawatakuacha kirahisi.

Tembea katika kweli

“Yeye asemaye kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda.” 1Yohana 2:6. Kama tumeitwa na kuchaguliwa kwake, hivyo tumeitwa kuwa mfano hai wa ukweli. Neno la Mungu lazima lionekane ndani yetu. Watu wanapaswa waweze kuona neno la Mungu maishani mwetu. Lazima tuwe mfano hai wa ukweli na maisha yet una maneno yetu.

Tuanapaswa kutambua kwamba tumeitwa kutenda. Tunapaswa kujua kwamba Mungu ni baba yetu, tunapaswa pia kuwa “wafalme wa ukweli” tulioitwa tutawala na kushinda nguvu zote za tuhuma, kudanganya, kusifia, na unafiki. Tunawezaje kama wafalme wa ukweli, kutambaa mbele ya watu na kuwasifia ili kupata nafasi nzuri ulimwenguni, au kutosema ukweli wote ili tufaidike na watu wasifikirie vibaya dhidi yetu? Hapana, mfalme wa ukweli lazima aishi na kutembea katika ukweli.

Watu wengi hupoteza hamasa juu yetu tunapokuwa wakweli na waaminifu kila wakati. Huwa tunapoteza kila kitu kinachoonekana kuwavutia watu, kwa kuwa hiyo inatoka kwa shetani. Tunakuwa wa asili na wanyoofu, na tunapoteza kila kitu cha ambacho watu wa dunia hutamani na kutegemea. Lengo la mkristo wa kweli ni kupotelea kwenye usuli ili yeye mwenyewe asiwe kitu chochote, lakini Kristo huwa mkuu kwa kila jambo afanyalo na kunena. “Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na kristo katika Mungu.”  Wakolosai 3:3.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye Makala ya Aksel J. Smith ambayo mwanzoni ilionekana ikiwa na kichwa cha Habari “Kwa sababu hii nilizaliwa” kwenye jarida la BCC “Skjulte Skatter” (“Hazina zilizofichika”) Mei 1934. Imetafsiriwa kutoka Kwenye Kinorwe na imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika kwenye tovuti hii.