Ndoa safi

Ndoa safi

Usafi ni jambo ambalo linazidi kuwa la kawaida.

27/6/20133 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Ndoa safi

5 dak

Je, inawezekana kuwa na ndoa safi, ambapo unakuwa mwaminifu kwa mwenzi wako wa ndoa katika mawazo na matendo?

Usafi ni kitu ambacho kinazidi kuwa si cha kawaida katika ulimwengu huu. Hata Wakristo wengi hawaamini kabisa kile ambacho Biblia inasema kuhusu hilo, wala wengi wao hawaishi maisha safi. Aina nyingi za uasherati hazizingatiwi kuwa dhambi tena.

Tunaposoma kile ambacho Yesu Mwenyewe anasema kuhusu usafi, tunaona kwamba ni zaidi ya kuwa msafi katika matendo, msafi kwa nje. Yesu alitufundisha kinyume cha moja kwa moja cha yale viongozi wa kidini wa wakati huo waliyofundisha, ambao walionekana wasafi kwa nje lakini ndani walikuwa wamejaa uchafu wote. ( Mathayo 23:27 ) Hawakutaka kufanya jambo fulani kuhusu uchafu uliokuwa ndani yao.

Ndoa safi huanza na maisha ya fikra safi

Yesu alisema kwamba mtu anayemtazama mwanamke kisha anafikiria kufanya naye dhambi ya ngono, tayari amefanya uzinzi naye moyoni mwake. (Mathayo 5:20, 27, 28.) Hii inaonyesha kwamba ni mawazo yetu tunayohitaji kuyaweka safi kutokana na aina zote za tamaa ambazo tunazo ndani ya asili yetu potovu.

Kujamiiana ndani ya ndoa ni jambo ambalo Mungu amekusudia liwe baraka, lakini Yesu anaweka wazi kuwa hata kuwa na mawazo ya kumtamani mtu mwingine tofauti na mwenzi wako wa ndoa ni dhambi. Hatuwezi kujizuia kuona au kusikia mambo katika ulimwengu unaotuzunguka, lakini tunapaswa kujifunza kusema Hapana kwa uthabiti wakati mambo ambayo tunaona na kusikia yanapoamsha tamaa za dhambi katika maisha yetu ya mawazo.

Hivyo ndivyo Yusufu alivyofanya. Mke wa Potifa alipojaribu kumshawishi, alimkataa. Aliwezaje? Jibu ni katika kile alichomwambia – "Nifanyeje ubaya huu mkubwa nimkosee Mungu?" Mwanzo 39:9. Badala ya kushindwa na majaribu, alikimbia na kujiweka safi.

Ni hofu yako ya Kimungu ambayo haitakuruhusu usiwe mwaminifu, iwe ni katika mawazo yako, mahali unapotazama, au katika matendo yako. Unapokuwa na hofu ya Mungu, inakupa akili thabiti, na yenye maamuzi. Kisha unafanya uamuzi thabiti wa kukaa mbali na kila kitu ambacho ni kichafu, hata unapokuwa kwenye mitandao ya kijamii au uperuzi kwenye mtandao.

Hata utakapoamua kwa uthabiti kukimbia kama Yusufu, bado utajaribiwa na uchafu kwa sababu ya tamaa katika asili yako ya kibinadamu. Kujaribiwa sio dhambi, lakini ni mtihani wa uaminifu wako. Lazima uchague kutawala dhambi ambayo unajaribiwa nayo. Hii ina maana kwamba unapojaribiwa, unapaswa kupinga na kupigana na mawazo machafu yanayotokea na kumlilia Mungu ili akusaidie. Mungu atasikia kilio chako na kukupa uwezo wa kushikilia uamuzi wako wa kujiepusha na uchafu.

Ukiendelea kufanya hivi, utapata uzoefu wa jinsi Mungu anavyokubadilisha kuwa mtu mpya kabisa na aliye huru.

Ndoa inatoka kwa Mungu

Siku hizi, watu wengi huona ndoa kuwa ni jambo la kizamani, lakini sivyo Mungu anavyoiona. Mungu Mwenyewe huona ndoa kuwa muhimu sana kiasi kwamba Biblia hutumia mfano wa ndoa safi kufafanua uhusiano safi, mtakatifu na mkamilifu kati ya Kristo na kanisa Lake.

Wenzi wa ndoa wanapokosa uaminifu kwa kila mmoja wao, husababisha maumivu, mashaka, na taabu kwa wenzi wao wa ndoa, watoto wao na kila mtu mwingine anayehusika. Ndoa inapaswa kuwa mahali pa usalama, uaminifu, na upendo safi ambapo Mungu anaweza kutoa baraka zake.

Zaburi 110:2 inaamuru, "uwe na enzi kati ya adui zzako!" Uchafu ni mojawapo ya "maadui" ambao tunapaswa kuwatawala katika mawazo yetu. Ni vizuri jinsi gani kujua kwamba inawezekana kukataa tamaa za ngono katika mawazo yetu, ili zisiharibu akili zetu au kuharibu mahusiano yetu! Na hii inaleta baraka kubwa kutoka kwa Mungu!

Chapisho hili linapatikana katika

Makala haya yanatokana na makala ya Tony Jacobs yaliyochapishwa awali kwenye https://activechristianity.org/ na yamebadilishwa kwa ruhusa ya matumizi kwenye tovuti hii.