Kukesha na kuomba kuna maana gani?

Kukesha na kuomba kuna maana gani?

22/8/20173 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Kukesha na kuomba kuna maana gani?

4 dak

Kukesha na kuomba kunamaanisha kuamka na kuwa macho siku nzima ili tuweze kuona dhambi pindi dhambi inapongojea kwenye mlango wa mioyo yetu, kutaka kutukamata na kutushikilia. (Mwanzo 4:7) Inamaanisha kwamba tuna muunganiko wa moja kwa moja na Mungu; kwamba tunaenda kwake kwa nguvu kushinda dhambi zote tunazojaribiwa nazo.

Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho I radhi, lakini mwili ni dhaifu.” Mathayo 26:41

Lazima tuamke na kuwa macho. Daima shetani anasubiria fursa aje ndani. Ikiwa hatuko macho hata kwa muda kidogo tu, inampa wakati ambao alikuwa anausubiria. Hitaji la shetani ni kutugeuza mbali na Mungu. Ikiwa tutakesha kuomba, ndipo tutakapoweza kumpinga daima, imara katika Imani yetu, tukijua kabisa undugu wetu katika dunia hupitia aina moja ya kutuseka. (1 Petro 5:8-9.)

Tuna tamaa mbaya na matakwa katika asili yetu ya kibinadamu ambayo inataka kutuchukua kwenye vitu ambavyo havimpendezi Mungu. Tunaweza kuyashinda kwa nguvu ya Mungu. Yesu alipitia vitu sawa alipokuwa akiishi duniani. Aliomba kwa kilio cha nguvu na machozi kwa baba yake. Aliamka na kuwa macho zaidi hivyo dhambi haikuweza kupenya moyoni mwake. (Waebrania 5:7.)

Tunahitaji kuwa na muunganiko wa moja kwa moja na Mungu kuanzia muda tunapoamka hadi muda tunapokwenda kulala tena. Kwa kweli, hatuwezi kuwa tumepiga magoti siku nzima, na tuna mambo mengi ya kufanya, lakini tunahitaji kuwa na uhusiano na Mungu hivyo basi tunaweza kwenda kwa msaada ambao tunahitaji, kutafuta matakwa yake na kutafuta nguvu ya kutafanya. Silaha ambayo Yesu aliitumia, ili kushinda pindi alipojaribiwa, ilikuwa ni maombi na neno la Mungu. Shetani hana silaha ambayo inaweza kushinda silaha ambayo Mungu hutupatia.

Moyo wako ni kama bustani ambapo

Yesu hupanda mbegu zake.

Angalia hivyo shetani hawezi kuja na

Kupanda magugu mabaya”

Tunapokuwa macho na kuamka, tutaweza kuona pindi shetani anapojaribu “kupanda magugu mabaya” kwenye mioyo yetu. Ndipo tunahitaji kuomba kwa Mungu kutusaidia kuzitoa mbegu zote za uovu ili zisianze kuota kwenye mioyo yetu. Huwa daima hazionekani kama ni kubwa, Dhahiri ni dhambi. Mara nyingi shetani atajaribu kutuchota na vitu “visivyotisha”, dhambi ndogondogo ambazo hazionekani kama ni Dhahiri. Ni muhimu kuwa macho ili tuweze kuona majaribu madogomadogo kuwa ni ya hatari.

Fikiri juu ya hali zinazikujia na mazungumzo tunayoshiriki. Mawazo gani tunayaruhusu kuingia kwenye akili zetu siku hizi? Amka na uwe macho kwa shetani na magugu yake mabaya!

Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya kweli, staha, haki, safi, yenye kupendeza, yenye sifa njema; ukiwapo wema wote, ikiwapo sifa nzuri, yatafakarini hayo.” Wafilipi 4:8. Ikiwa hakika tunafanya kile kilichoandikwa kwenye mstari huu kila siku, Shetani hana nafasi ya kuingia ndani.

Haijalishi tunafanya nini, tunahitaji kukesha na kuomba ili tuweze kuweka mioyo yetu safi. Mungu alituita kwenye maisha haya ya ajabu! Lazima tusiruhusu chochote kuingia ndani na kuvujisha kile ambacho tumepewa.

Jamii
Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kutoka kwenye Makala na Philip McNutt, mwanzo ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org/ na ikabadilishwa kwa ruhusa kwa matumizi kwenye tovuti hii.