Kwa nini kuwa na uchungu husababisha shida

Kwa nini kuwa na uchungu husababisha shida

Uchungu na kuwa na jambo dhidi ya mtu mwingine huhwaweka watu mbali kati ya mmoja na mwingine – lakini kuna suluhisho.

12/8/20214 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Kwa nini kuwa na uchungu husababisha shida

Mfano wa Yusufu wa kusamehe

“Ndugu zake Yusufu walipoona ya kwamba baba yao amekufa, walisema, labda Yusufu atatuchukia; naye atatulipa maovu yetu tuliyomtenda. Wakapeleka watu kwa Yusufu, kunena, baba yako alitoa amri kabla ya kufa kwake, akasema, mwambieni Yusufu hivi, Naomba uwaachilie ndugu zako kosa lao na dhambi yao, maana walikutenda mabaya; sasa twakuomba utuachilie kosa la watumwa wa Mungu wa baba yako. Yusufu akalia waliposema naye. Mwanzo 50:15-17

Ndugu wa Yusufu waliogopa kwamba aliwasamehe kwa kuwa tu baba yake alimwambia kufanya hivyo. Mara nyingi, kama mtu angekuwa ametendewa mabaya kama Yusufu alivyotendewa na ndugu zake angekuwa na uchungu.

Sasa Yusufu alikuwa na nguvu ya kuwaadhibu, na ndugu zake waliogopa adhabu. Hivyo walimfuata, wakamwangukia, kusema, “sisi tu watumwa wako” Mwanzo 50:18. Lakini ndugu zake hawakuwa na sababu ya kuogopa. Yusufu aliuweka moyo wake safi kwa kila jambo hivyo angeweza kuona mkono wa Mungu kwa kile kilichokuwa kinatokea. Alikuwa maewasamehe kutoka moyoni, na hapa linakuja neno maarufu “Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo” Mwanzo 50:20.

Hii ni moja kati ya hadithi zenye kugusa ambayo tunaweza kuisoma katika biblia. Yusufu alitambua kwamba kuwasamehe ndugu zake na kuwa na amani pamoja nao ilikua muhimu sana kwa Watoto wa Yakobo pamoja na kizazi cha badae kuweza kukaa pamoja na kujitunza kama wamoja kwa badae. Hebu fikiria kwamba taifa hili lenye makabila kumi na mawili lilianza na ndugu 12  kuleta amani na kila mmoja.

Ushinde uovu kwa wema

Nelson Mandela Afrika kusini alitenda katika njia ile ile. Aliwekwa gerezani katika kisiwa cha Robben kwa miaka 27. Kwa uzoefu huu ungemfanya mtu awe na uchungu. Lakini aliopoachiwa kutoka gerezani, alisema, “Kwa kuwa nilitembea nje ya mlango kuelekea kwenye lango ambalo lingeniweka katika uhuru, najua nisingeacha uchungu na chuki zangu, ningekuwa bado nipo gerezani” Alitambua kwamba hatima ya watu nchini mwake isingejengwa katika uchungu lakini ingejikita katika msamaha na kuleta amani kati ya mmoja na mwingine.

“Usishindwe na ubaya, bali ushinde ubaya kwa wema”Paulo anaandika katika Warumi 12:21. Ikiwa unakuwa na uchungu katika hali za maisha, unakuwa umeshinda kwa uovu. Na hivyo hauna uwezo wa kuushida uovu.

“Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakaemwona Bwana asipokuwa nao; mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.” Waebrania 12:14-15. Shina hili la uchungu linaweza kukua katika uchafu au moyo usio safi. Husambaa kwa watu wengine, na huleta uharibifu tu. Lakini moyo safi huondoka uchungu.

Msalaba huunganisha

“…Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno ya upatanisho” 2Wakorintho 5:19. Kwa kupitia kifo cha Yesu kunaweza kuwa na upatanisho kati ya Mungu na dunia. Upatano unaweza kuonekana kwa kila nafsi ambayo huamini katika Kristo.

“Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. …….. Kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba” Waefeso 2:14-16.

Kama binadamu huwa tunakumbuka kirahisi sana mabaya yote ambayo wengine wametutendea. Lakini ikiwa tunataka kuleta amani ambayo Yesu aliileta, tunapaswa kuyaweka yote haya “msalabani”. Hii inamaana kwamba dhambi zetu lazima “zisulubiwe” lazima “Zife” na zisiongoze matendo yetu tena. “Msalaba” ni mahali pekee ambapo chuki na uchungu vinaweza kuuawa.

Chuki na uchungu huwatawanya watu, wakati msalaba huwaunganisha watu. Ikiwa unazungumza uovu wa mtu fulani au kumlaumu mtu Fulani, ni chuki katika asili yako ya kibinadamu yenye dhambi ambayo inatumia ulimi wako kama chombo. “Tulikua tukiishi katika uovu na husuda . tukichukizana na kuchukiana”Tito 3:3. Chuki hupelekea chuki Zaidi. Fikiria kwamba tunaweza kutoka katika duara la uovu milele! Hivyo inafaa kwetu kama wakristo, “Msimtukane mtu ye yote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote.” Tito 3:2. “……Kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo hivyo na ninyi.” Wakolosai 3:13.

Tunaona kwamba msamaha na kupatanisha mmoja na mwingine ni moja kati ya msingi na jambo muhimu katika mafundisho ya kikristo na pia kigezo cha kuwa mjenzi wa jamii.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita katika Makala ya Øyvind Johnsen awali ilichapishwa katika https://activechristianity.org/ imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika katika tovuti hii.