Kwa nini ni muhimu kuweka mambo rahisi

Kwa nini ni muhimu kuweka mambo rahisi

Tusimruhusu shetani afanye mambo kuwa magumu kwetu.

1/6/20194 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Kwa nini ni muhimu kuweka mambo rahisi

7 dak

Mungu ameotesha miti miwili maalumu kwenye bustani ya Eden: ‘Mti wa uzima’ na ‘mti wa kujua mema na mabaya’. Mungu aliwaambia Adam na Eva kwamba hawakupaswa kula katika ‘mti wa kutambua mema na mabaya’, lakini wangeweza kula kila watakacho katika ‘mti wa uzima’. Ni sawa hata kwetu, “ Nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya.” Warumi 16:19.

Hatupaswi kuruhusu uovu ututawale


Mungu anajua jema na ovu, lakini uovu haumtawali. Hii ndio asili kiungu ilivyo. (Mwanzo 3:22.) Lakini kama binadamu wa asili tu wadhaifu sana kiasi kwamba huruhusu uovu ututawale kirahisi. Mungu anataka kutuweka mbali na uovu kwa kuwa anatupenda sana. Njia pekee ambayo Adam na Eva wangewekwa mbali na uovu ilikuwa ni kutii amri za Mungu kutokula kutoka kwenye ‘tunda la mem ana mabaya’.

Leo pia ni mapenzi ya Mungu kwamba tusiruhusu uovu ututawale.Mapenzi yake ni kwamba si kwamba tupokee tumsamaha wa dhambi, lakini tuweze kuushinda kabisa uovu.

Shetani pia anatambua hili. Alimlaghai Eva kula katika mti wa maarifa, kumdanganya na kusema kwamba angeweza kuwa kama Mungu na angejua tofauti kati ya mema na mabaya na asingekufa, kwa kuwa Mungu hafi japo anajua mema na mabaya. Alimlaghai Eva kwa kumfanya asitii neno la Mungu ionekane kama jambo jema, au jambo ambalo lingemfanya awe mjanja. Ni sawa hata leo. (Mwanzo 3:4-5.)

Shetani alimlaghai Eva kuzitilia shaka amri za Mungu. Kwa kuzitilia shaka alianza kwenda mbali na mapenzi ya Mungu, ambayo ilikuwa ni kutii amri yake ya kutpokula kutoka kwenye mti wa maarifa. Tofauti kati ya mema na mabaya ikawa giza na isiyoeleweka na Eva alitenda dhambi. (Waefeso 4:14; Wagalatia 5:10; 1Timotheo 2:14.)

Upendo rahisi wa Kristo

Lakini nachelea, kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikra zenu, mkauacha unyofu wa Kristo.” 2Wakorintho 11:3. Ni upendo rahisi na mtakatifu kwa Kristo ambao huweka fikra zetu mbali na uongo wa kidini na mkanganyiko katika siku hizi. “Mkinipenda, mtazishika amri zangu” Yohana 14:15. Huu ni urahisi wa kimbingu.

Japokuwa Wagalatia walikubali mafundisho ya Paulo mwanzoni kwa furaha, walidanganywa na kupoteza njia yao. Inayoitwa “muhimu” au mitume waliwapelekea Wagalatia kufikiri kwamba haikiuwa lazima “kusulubiwa” na Yesu kila siku- kwamba hawakuhitaji kusema hapana kwa matamanio yao ya dhambi kila siku. Walifikiri wangeweza kuokolewa kirahisi zaidi pasipo kuifanya. Kila kitu kingeweza kuwa sawa endapo tu wangeweza kutakaswa kimwili. Hii iliubiriwa kwao kwa siku hizo. (Wagalatia 5:10; 2 Wakorinto 11:5).

Leo inahubiriwa kwamba kila kitu ni sawa ikiwa tu tunaamini kwamba Yesu amefanya kila kitu kwa sehemu yetu. Tunachokifanye sio tena cha muhimu. “Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulubiwa”.

Kwa Paulo Yesu hakusulubiwa tu Kalvari lakini pia ni “Mtangulizi” (Waebrania 6:20) ambaye ameubeba msalaba wake kila siku,daima alisema Hapana pale alipo jaribiwa kutenda dhambi. Wote wanaomfuata hufanya vilevile. “Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate.” Luka 9:23.

Soma Zaidi hapa kuhusu maana ya kubeba msalaba wako kila siku.

Roho ya kimungu ilimwambia Yesu kubeba msalaba wake kila siku, na roho inatuambia kufanya sawa leo, na anatufundisha kuifanya kwa furaha. Hii hututia moyo, huifanya Imani yetu kuwa yenye nguvu na hutusaidia katika majaribu kuchagua matakwa ya Mungu na kubadilika kama mwana.

Hatuwezi kuwa pasipo matendo (Yakobo 2:14,17), kwa sababu kama sisi, tutapoteza nguvu ya Mungu na pia wokovu wa nafsi zetu. Ambapo hatuna matendo, ni kama tunaishia kuwa na aina fulani ya utauwa, maisha yasiyo na ushindi dhidi ya dhambi.

Shetani ana akili sana na ni mdanganyifu. “Kuweni thabiti katika imani na mpingeni,” imeandikwa katika 1 Petro 5:9. Huo ni uhalisia wa kimbingu! Lazima tuamke katika mawazo yetu kimaisha; fikra zetu zinatakiwa ziwe safi pasipo kujali kipi hutokea hivyo basi yesu ni pendo letu pekee. Ndipo hatuwezi kutii roho nyingine au injili nyingine ambayo hatukuipokea mwanzo. (Yakobo 2:14,17; 1 Wakorontho 1:17-18;; 2 Timotheo 3:5; 2 Wakorintho 11:2,4)

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita katika Makala ya Jaap G. Littooji ambayo awali ilionekana chini ya kichwa cha Habari “ Urahisi wa kimbingu” kwenye jarida la mara kwa mara la BCC “Skjulte Skatter” (Hazina zilizofichika) juni 2021. Imetafsiriwa kutoka kwenye Kinorwe na imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika kwenye tovuti hii.