Siri ya mahusiano mazuri

Siri ya mahusiano mazuri

kufuatilia masomo haya matatu yatakusaidia kuwa na mahusiano mema, yenye baraka na afya!

23/4/20195 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Siri ya mahusiano mazuri

Mahusiano si rahisi kila mara. Watu wanatofautiana kutoka mmoja kwa mwingine. Namna mtu mmoja anavyofikiria ni tofauti kabisa na mtu mwingine anavyofikiria. Watu pia hutofautiana katika njia ya kuwasiliana.

Mungu alimuumba kila mmoja wetu na karama na ujuzi tofauti, na tunaweza kuwa wenye shukrani kwa kila mmoja wetu kwa nguvu tofauti. Kila mmoja kati yetu pia ana nafasi katika asili yetu ambapo ni mdhaifu kiasili, maeneo ambayo tunaweza kuendelea. Matokeo yake, kuna mambo mengi tunaweza kujifunza kutoka kwa kila mmoja wetu maishani.

Somo #1: Napaswa kuzingatia maeneo ambayo nahitaji kubadilika

Somo moja ambalo litanisaidia kuwa na mahusiano mazuri ni kwamba nahitaji kuwa na uhusiano wangu mwenyewe na Mungu katika maisha, na kuzingatia kile ambacho Mungu anataka nifanye katika hali tofauti tofauti badala ya kile ambacho wengine wanafanya. Watu wengi wanafahamu kifungu kwenye Mathayo 7:1-2: “msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho ndicho mtakachopimiwa.” Kwa hiyo swali kwangu ni je napaswa kufanya hivi kwa maisha yangu, ya kila siku?

Najua kwamba namna navyoona mambo si kama mtu mwingine anaweza ona katika hali hiyohiyo. Na hata kama mawasiliano yanapokuwa mazuri, bado inawezekana kutoelewana na kuhukumu vibaya. Hivyo Mungu alipotupa amri hii, haikuwa kwa sababu kuhukumu wengine hupelekea aina zote za uovu, kama kukosoa, kutuhumu na kusengenya. Ilikuwa pia kwa sababu hukumu yangu si ya kweli na ya haki kila mara.

“Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? Au utamwambiaje nduguyo, niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.” Mathayo 7:3-5.

Nikizingatia pale ambapo mimi mwenyewe nahitaji kubadilika ninapojaribiwa kuhukumu na kukosoa, ndipo nitakapogundua kwamba nina kazi nyingi za kufanya ndani yangu mwenyewe.

Ninapokuwa pamoja na wengine, Mungu anataka kunionesha mambo kunihusu mimi , mambo yasiyokuwa yanavyopaswa kuwa. (Yakobo 1:4; 1Petro 5:10; Wafilipi 3:12.)

Kwa mfano, pengine ninapata wasiwasi kirahisi kuhusu yale watu wengine wanavyowaza juu yangu, kwa hiyo hutumia muda mwingi kuwa na hofu juu ya waliyosema ama kutenda. Mungu anataka niwe na furaha kamili na amani katika maisha yangu ya kila siku, na ni rahisi kuona kwamba kuwa na hofu kama hivi hakuleti furaha kamili na amani. Kwa hiyo Mungu anapaswa kunionesha tabia hii kupitia hali zangu za maisha ya kila siku, na ndipo niishinde.

Somo #2: Tunaweza kuwa na mtazamo sawa wa akili, bila kujali tofauti zetu

Yesu alikuja “kumaliza kile kilichokuwa kimeleta matabaka kati yetu”. (Waefeso 2:14-18.)  Katika agano jipya, imeandikwa jinsi wagiriki na wayahudi hawakuelewana kabisa kwa kuwa walikuwa tofauti kabisa kati ya mmoja na mwingine – walitofautiana kimila, kiutamaduni na Imani tofauti. Hawakuweza kuelewana kabisa kati ya mmoja na mwingine. Lakini Mungu aliibadili hali hii alipokuja na ujumbe wa “msalaba”, unaotufundisha kushinda tamaa na mahitaji ya asili zetu wenyewe za dhambi.

Soma Zaidi kuhusu ujumbe wa msalaba hapa : Ujumbe wa msalaba: ukristo wa vitendo

Kuisema kwa kirahisi, lengo ni kuitikia kwa wema, ukarimu, na upendo dhidi ya watu ninaokutana nao. Katika vitendo, hii inamaanisha napaswa kushinda kila jambo ndani yangu na yanayonizuia mimi kutenda hivyo. Hiyo inaweza kuwa ubinafsi wangu, ubinafsi wangu na maoni yangu, hofu, kukosa uvumilivu, kuogopa dhidi ya watu wanavyofikiria, n.k.

Hivyo hata kama watu wanatofautiana, njia hii ya kushinda tabia na mahitaji yetu ya dhambi inaweza maliza “matabaka” yote na ugomvi na inaweza kutupelekea kuwa na mtazamo sawa wa kiakili: tuna lengo sawa – kushinda tamaa na mahitaji ya dhambi ambazo hututenga na Mungu na kutufanya tusiwabariki wengine. (Waefeso 2:22)

Somo #3: Wakati mwingine napaswa kunyamaza

Kabisa, si kila mmoja huamini katika “ujumbe wa  msalaba”,  na wakati mwingine tunakuja katika hali ambapo watu (iwe kwa kumaanisha ama kutoamaanisha) hutuumiza ama ni wakali. Katika hali hizi, ni muhimu kusikiliza kwa makini Mungu anazungumza na mimi.

Wakati mwingine ni haki kupaza sauti na kuongea kile kinachopaswa kuongelewa, au angalau kuelezea maoni na kwa nini unaona au kuelewa mambo tofauti. Wakati mwingine ni muhimu kusimamia ukweli, na wakati mwingine kusema ninachodhani ni muhimu kwa ajili ya mawasiliano mazuri.

Wakati mwingine, na hii ni mara nyingi baada ya kuelezea “Kwa upande wangu” mambo nayojua kabisa kwamba Mungu ananiambia “kunyamaza sasa”. Hufanya kazi ndani yangu kuwa mwema dhidi ya mtu ambae sikubaliani nae ama kumhukumu.

Nikiwa nina shauku katika kushinda tabia zangu za dhambi badala ya kutaka wengine wabadilike, ndipo nitakaposema kwa uaminifu “Hapana” kwa mawazo ya uchungu, mawazo ya hukumu ya ukali, au kuanza kuwasema ama kuwaadhibu wengine. Inamaanisha kwamba ninazingatia yale ambayo Mungu anataka kunifundisha katika kila hali: ninazingatia kuguswa na neno lake na mapenzi yake.

Kila dhambi huanza na wazo, hivyo kuitikia katika njia ya haki, ninapaswa kuhakikisha kwamba siruhusu mawazo yoyote ambayo hayampendezi Mungu kubaki moyoni mwangu. (2 Wakorintho 10:5)  nikiendelea kufanya hivi, mahusiano yangu yatakuwa mazuri Zaidi na Zaidi, na nitakuwa baraka kwa wote wanaonizunguka.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye Makala ya Page Owens awali ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org/ na imechukuliwa na kupewa ruhusa ya kutumika kwenye tovuti hii.