Makini, lakini bila hofu

Makini, lakini bila hofu

Mwanzoni kujitenga na kuunganishwa kwa njia ya mtandao ilikua kitu kigeni na pia chenye kufurahisha – mpaka nilipogundua kwamba vyanzo vyetu vya mapato vilikua vikipungua kwa mmoja hadi mwingine.

28/4/20204 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Makini, lakini bila hofu

7 dak

Mwanzoni mwa mwezi Aprili taarifa ilichapishwa katika utafiti wa kampuni ya kiitaliano iitwayo AI Company Expert System. Walikuwa wakifanya utafiti katika makumi ya maelfu ya machapisho ya mitandao ya kijamii ili kuweza kuangalia mabadiliko ya hisia katika jamii kuhusiana na virusi vya Korona. Walichokigundua hakikua cha kushtusha; Siku ya nne mfululizo hofu ndiyo ilikuwa imetawala katika machapisho mengi. “Kuna sababu nyingi zinazopelekea hofu kukua” Timu iliandika katika taarifa ya siku.

Ndiyo kuna sababu nyingi za kukufanya uwe na hofu, kuwa mwoga kuhusu kile kinachotokea. Taarifa ilipendekeza kwamba mbali na mawazo juu ya kifo, hofu hutokea pale ambapo haujui mpango wa kutafuta suluhisho ama serikali itavyoweza kutafuta suluhisho.

Kuwa mtulivu

Kuna wakati ningesoma taarifa hizi na kuwaonea huruma hawa watu wasio na bahati ambao hawakumwamini Mungu, hawakuwa na imani katika “maisha ya badaye” ambayo yangekuwa ngao dhidi ya hofu kwa maisha yajayo.

Nilihisi hivi kwa sababu nimekuwa mwanamke mwenye kuridhika ambaye angeweza kutaja vifungu vizuri kwa waumini wengine kwa wakati mgumu. Vifungu kama:

“Msijisumbue kwa neno lolote….” Wafilipi 4:6-7

Nilikua nikipata msaada kutoka kifungu hicho kwa sababu ni amri: Hakinipi nafasi ya kuchagua. Kinaniambia cha kufanya – Nimwombe Mungu katika mahitaji yangu– Na kinaniambia kitakachotokea – Kwamba amani ya Mungu itakuja moyoni mwangu na akilini mwangu.

Nimekifanyia kazi kifungu hiki na imenibidi nifanye hivyo. Kimenisaidia mara nyingi sana kutokana na wasiwasi ambao hujaza mioyo yetu panapotokea tukio la ghafla ambalo halikutarajiwa.

Nilikua na imani hii kwamba ili mradi ningekua mwanafunzi, niliamini kwamba Mungu alikua na mimi kwa lolote lililotokea. Nilikuja kuwa mtaalam katika hili. Nilijua namna ya kupambana na hali ngumu, na nilifikiri nilikua nimeelewa kweli, na kwa hiyo niliweza kukirudia kifungu hiki kwa watu wengine bila kuchunguza zaidi matatizo yao.

Sasa licha ulimwengu unavyolichukulia suala la virusi linaloua watu wengi haraka, Nimehisi utulivu. Najua kwamba hakuna kinachoweza kugusa nywele za kichwani mwangu isipokuwa Mungu aruhusu. Na hili ni pamoja na familia yangu. Nilijihisi mwenye utulivu, lakini bila hofu.

Pigo la kweli

Lakini marufuku ya kutoka ndani Uingereza yakatokea, Mwanzoni kujitenga, ukweli kwanza tusingeweza kutembea mahali popote, na kuungana na marafiki, wenzetu na wanafunzi kwa njia ya zoom ilikua kitu kipya na cha kufurahisha – hadi nilipogundua kuwa kwa sababu wanafamilia katika nyumba yangu wamejiajiri, vyanzo vya mapato yetu vimekatika mmoja baada ya mwingine. Wateja wa mume wangu hawapo tena, wagonjwa wangu hawahudhurii miadi, Mwanafunzi wa mwanangu hawezi kuja tena kufundishwa kinanda.

Na kama mtu amepanga katika jengo letu hawezi kulipa kodi kwa sababu haendi kazini – hiyo itakua pesa ya ziada tunatakiwa kulipa benki kutoka katika kipato chetu kinachopungua kwa kasi.

Ghafla hofu ikanipiga kwa nguvu na bila kutegemea – na kwa kasi ikanitoa katika hali yangu ya kuridhika kwamba hofu nilikuwa naitawala. Ghafla mawazo yangu yalikua: Tugeweza kupoteza nyumba yetu, kupoteza mafao yetu, na kupoteza biashara zetu.

Sikuwahi tarajia kama ningeweza pata pigo kiasi hiki. Mimi ni mwanafunzi wa Yesu. Najua maisha yangu yako mikononi mwa Mungu. Sitikiswi na vitu vinavyowapa hofu wengine ambao hawana imani.

Hivyo kweli naishi kwa kufuata andiko hili- usihofu kuhusu chochote? Inashangaza kwamba sikujaribiwa kuwa na hofu kuhusu virusi vinavyoshambulia mwili wangu, lakini nakua na hofu kuhusu kupoteza nyumba yangu.

Kuna kitu kimoja sipaswi kukipoteza kamwe

Nilihitajika kufikiria kwa umakini sana. Kipi kibaya kinachoweza kutokea? Vipi kama nikifa? - Naenda kuishi na Yesu. Kama nikipoteza biashara yangu? - naweza kutafuta kazi nyingine. Tukipoteza nyumba yetu? Tunaweza tafuta kitu kidogo. Ah, Lakini je, nikipoteza imani yangu? - hicho ndicho kitu kibaya zaidi kinaweza kutokea.

Imani yangu lazima ijaribiwe ili niweze kuhimili mitikisiko ambayo hutokea kama matokeo ya majaribu na hali ngumu. Nisipopitia majaribu, hivyo siwezi kuupata ushindi. Naweza nisifahamu kitakachotokea kwangu ama kwa familiya yangu; Sijui ni uelekeo upi Mungu atatupeleka katika afya yetu, hisia au masuala ya kifedha, lakini nafahamu kuwa imani yangu lazima iwe thabiti.

Ndiyo, Nilishangaa kwamba nilijaribiwa kuogopa, lakini ilitakiwa nishangae? Hali hii imeniamsha na kunikumbusha kuwa mwangalifu zaidi: kutambua hisia hizi za kidanganyifu, kufikiria kuhusu vitu ambavyo naweza mwambia mtu yeyote kirahisi, Kujaribu kukubaliana na ambao ni waoga na wasio na uhakika. Hii imenitoa katika ukanda wangu wa utulivu na hivyo ni vyema. Chochote kinachoijaribu imani yangu ni kizuri kwangu. Katika nyakati hizi zenye mashaka, kumwamini Mungu ndicho kitovu cha maisha yangu, siku yangu, na fikira zangu, kwa sababu bila hayo naweza poteza kila kitu.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita katika makala ya Maggie Pope awali ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org/ na imeruhusiwa kuchapishwa katika tovuti hii.