Mambo yanapoenda vizuri kwa wengine

Mambo yanapoenda vizuri kwa wengine

Mambo yote hutokea kwa ajili ya mema kwangu” lakini je, ninalifanyiaje mazoezi katika maisha yangu ya kila siku, kama napojaribiwa kuwa na wivu?

15/8/20213 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Mambo yanapoenda vizuri kwa wengine

4 dak

“Mambo yote hutokea kwa ajili ya mema kwangu” ni jambo ambalo kila mkristo husikia. Kitu cha kushangaza ni kukubali! Sisi ni watu wenye bahati ambao tunaweza kuamini hili.. lakini je, nalifanyia vipi mazoezi katika maisha yangu ya kila siku, kwa mfano ninapojaribiwa kuwa na wivu? Nitawashirikisha hali niliyokuwa nayo hivi karibuni.

“Maisha ni kila kitu ambacho nilikua na ndoto kingekuwa” mmoja kati ya rafiki zangu alisema katika chapisho la facebook. “mmm.. Baadhi walionekana kuwa nayo, sivyo?” ilikua hisia yangu ya kwanza niliposoma hii. Kazi nzuri. Afya. Pesa. Mume. Watoto wapendwa. Talanta. Siwezi sema hali yangu ya kwanza ni kuwa na furaha dhidi yao. “kwa nini niwe na furaha juu ya mafanikio ya wengine – wakati nikihisi ndoto zangu zimetokomea?” hisia hizi zina nguvu sana. Nahisi kuwa na hasira.

Kama nilivyokaa pale na hisia hizi na fikra zilikuja, nasalis ala fupi, “Munu nisaidie, sitaki kuwa hivi!”

Hivyo nilikumbuka kifungu kifupi ambacho rafiki alinishirikisha miaka iliyopita, “Basi nyenyekeeni chini ya mkono ulio hodari..” 1Petro 5:6. Nafikiria juu ya maneno hay ana nina shauku ya kuwa mtiifu kwake. Natambua kwamba utii katika neno la Mungu utanipeleka kwenye amani na furaha kuu, maisha ambayo hayayumbishwi, bila kujalisha hali yangu ilivyo! Najua kwamba nipo mikononi mwa Mung una kila jambo linalotokea ni kwa ajili ya wema kwangu.

Kugeuzwa kutoka kwa kile cha kidunia kuwa kile cha kimbingu.

Nachagua kusema “Hapana”kwa fikra hizo za kulalamika, wivu, kujionea huruma, na kujua ndani yangu kwamba Mungu ana furaha na mimi. Fikra huanza kuja: kwa nini nisifikirie kuwatendea mema wengine? Hakuna watu ambao wapo vibaya Zaidi yangu kuliko nilivyo? Kwa nini unajifikiria mwenyewe?” macho yangu humtazama mmoja baada ya mwingine, watu tofautitofauti huja akilini mwangu – mahitaji yao ni makubwa kuliko yangu. Huanza kuwaombea, hutuma jumbe zenye kufariji, hupata maoni juu ya kile kinachoweza kuwa kizuri kwao. Moyo wangu hufunguka kuwahusisha wengine na kuwajali! Sijifikirii mwenyewe tena.

Je haya si maisha mazuri aliyoishi Yesu? Hakuja kutumikiwa lakini kutumikia na kutoa maisha  yake.  Fikiria ni kiasi gani niliyo na bahati! Ninaweza kumfuata na sihitaji kusihi kwa kufuata fikra za asili na hisia ambazo mara nyingi huleta huzuni, lakini badala yake naweza kutenda memq na kueneza baraka.

Biblia pia inatwambia kuwa na furaha na wale wafurahiao, na nimejionea hili tayari kwa kiasi Fulani. Hunileta katika maisha yenye furaha isiyo kifani, hata kama sina kila kitu ambacho rafiki yangu anacho. Macho yangu yageuzwe kutoka kwenye vitu ambavyo ni vya kidunia na kuja kwenye vitu vile vya kimbingu – ambavyo huleta pumziko la kweli na furaha. Neno la Mungu ni kweli.

“Kama unataka kufurahia maisha na kuona siku nyingi zenye furaha, uache mabaya na utende mema. Tafuta amani na uitafute sana” 1 Petro 3:10-11.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye Makala ya Gillian Savage awali ilichapishwa katika https://activechristianity.org/ imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika katika tovuti hii.