Nini maana ya kutembea kwa roho

Nini maana ya kutembea kwa roho

Ninawezaje kutembea kwa roho?

4/3/20115 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Nini maana ya kutembea kwa roho

Paulo anaandika katika Wagalatia 5:16, “Lakini nasema, Enendeni kwa roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.” Mwili ni usemi ambao biblia hutumia kwa asili zetu za mwili yenye dhambi pamoja na tamaa zake za ubinafsi – mambo hayo yote ndani yetu yanakwenda kinyume na Mungu na mapenzi yake.

Ubinafsi wetu ni kama kituo cha amri ambacho hutuma “ujumbe” mwingi. Jumbe na matendo yanayotokana na ubinafsi wetu yanatuhusu sisi wenyewe – kama vile kujifikiria wenyewe, kuwadharau wengine, kusema uongo ili kupata faida, kujaribu kupata sifa na kibali, kuwafanya watu watutambue, n.k. Hii ni tamaa y mwili, au tamaa za asili yetu ya dhambi na asili yetu ya kibinadamu ina mahitaji yasiyoisha.

Labda tunaweza kudhibiti tamaa hizi za dhambi kwa kiwango fulani, lakini kwa sehemu kubwa, asili ya mwanadamu inatawaliwa na tamaa hizo za dhambi. Ndiyo maana watu wanapotenda dhambi huwa tunawasikia wakisema, “Sisi ni wanadamu tu!”

Lakini Paulo aliandika kwamba ikiwa tutaenenda kwa roho, hatuhitaji tena kutekeleza tamaa hizi. Unapotembea kwa roho, unafikiri na kutenda tofauti na watu wengine katika hali za maisha.

Tembea kwa roho

Unapotembea unaanzia mahali fulani kisha unasonga mbele. Ukitaka kuenenda kwa roho, kwanza unahitaji kupokea roho. Roho tunaemzungumzia hapa ni roho mtakatifu. Roho mtakatifu ni nguvu halisi – halisi kama vile korongo inapoinua mzigo mzito kutoka kwenye meli hadi nchi kavu. Ikiwa unapata nguvu hii katika maisha yako, ni mwanzo wa sehemu mpya na ya kuvutia sana ya maisha yako.

Watu wengi wanaopokea roho hii wangependa tu kufurahia nguvu walizopokea, kama vile mtoto anayetaka tu kucheza. Lakini roho mtakatifu si kitu cha mchezo. Yeye ni msaada kwa watu wanaotaka kufika mahali fulani katika matembezi yao ya kristo.

Roho mtakatifu hutupatia nguvu ya kubeba mizigo mikubwa na magumu. Pia ni kiongozi. Anajua njia ambayo inatupeleka mbali na kila kitu ambacho ni hatari na hasi, kuelekea kile kilichobarikiwa na chema kwa wale wanaotuzunguka. Roho hutujaza furaha na amani. Tunakuwa na furaha ya kweli, na wale wanaotuzunguka wanaona hili.

Roho atatukumbusha na kutupa nguvu

Sisi sote tuapitia magumu maishani. Ni nani ambaye hajahisi kuwa kinachotokea sasa ni “cha kusikitisha na hakina maana”? Labda umepoteza simu yako ama pesa zako, au labda rafiki mzuri. Labda mtu amekusengenya, au hukupata kazi nzuri uliyoomba. Kuna mifano mingi, lakini nini kinatokea ikiwa tunatembea kwa roho?

Yesu anasema kwamba Roho anatukumbusha mambo yote aliyotuambia. (Yohana 14:26.) Kwa mfano kilichoandikwa katika Mathayo 6:34. “Basi msisumbukie ya kesho.”kuhangaika ni tofauti na kupanga siku yako, wasiwasi unakuelemea, unaiba nishati na furaha yako.

Roho hutukumbusha kuhusu kile alichoandika Petro, “Huku mkimtwika yeye fedheha zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha na sana kwa mambo yote”. Tunapotembea katika katika roho, maneno haya huenda moja kwa moja ndani ya mioyo yetu na kuwa nguvu ambapo tunasema hapana kwa mawazo yote ya hofu ambayo huja. Roho hutuhutupa nguvu ya kufanya hivyo, katika njia sawa na korongo ambayo huinua tani nyingi za bidhaa kutoka katika meli hadi nchi kavu.

Kutembea katika roho ni kuwa mtii wa roho

Kutembea katika roho inamaanisha kuwa mtii kwa roho – sheria na amri ambazo roho inatukumbusha tunapojaribiwa. Kujaribiwa si sawa na kutenda dhambi, lakini unapojaribiwa una chaguo na wewe mwenyewe unapaswa kuamua nini unaenda kufanya. Mtu anaposema jambo la kukuumiza au la kifidhuri kwako, kila mmoja anajua aina gani ya mambo unayojaribiwa nayo: kulipa ubaya kwa uovu na kumrudishia mtu huyo. Lakini ukifanya hivyo, unavunja amri za Mungu. Hiyo ni dhambi

Lakini roho mtakatifu anasema nini? “Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.” Warumi 12:21. Ukitembea katika roho, unafanya kile ambacho mstari huu unasema na unashinda dhambi. Kisha matokeo yake ni kwamba unapata furaha moyoni mwako, badala ya kusababisha maouvu zaidi.

Kutembea katika roho huzaa matunda.

Ukitembea katika roho, kitu cha kushangaza hutokea. Ambacho biblia hukiita “matunda ya roho” huanza kukua katika maisha yako – amani, furaha, uaminifu na wema kati ya mengi. (Wagalatia 5:22) Ambapo awali ulikuwa hujatulia, ukiwa na wasiwasi na mara nyingi huna furaha sasa unapata mtazamo unaofaa, furaha inakuwa sehamu ya maisha yako. Hauna tena wivu dhidi ya wengine.

Unapowapenda wengine, unajiepusha na mahitaji yasiy na kikomo ya mapenzi yako mwenyewe, na unaanza kufikiria kuhusu wengine na kile kinachoweza kuwa kizuri kwa wengine badala ya kuwaza kufikiria kuhusu wewe mwenyewe. Uaminifu unakuwa sehemu ya utu wako, na unakuwa mwaminifu katika kila unalosema na kutenda. Unakuwa mtu mpya. Si sahihi tena kusema, “Sisi ni wanadamu.” kiumbe kipya kabisa kinazaliwa katika maisha yako na kwamba nafikiri na kutenda tofauti na ulivyokuwa awali.

Matunda yote ya roho haya hukuwa unapotembea katika roho. Haya ni maisha ambayo Yesu aliyaishi duniani na ambayo unaweza kuyaishi kama mwanafunzi. Kutembea katika roho huchukua mazoezi. Wakati mwingine unaweza kufanya makosa, hususani katika mwanzo wa mtembeo wako wa kikristo, lakini hupaswi kupoteza ujasiri wala kudhani kwamba haina maana. Roho pia anaitwa “mfariji” katika tafsiri za biblia. Hutufariji sisi na kutupa ujasiri zaidi na ujasiri mpya tunapouhitaji.

Katika 2Timotheo 1:7 imeandikwa, “Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.” Tembea katika roho ndipo utakuwa na maisha yaliyotimia

Kuna watu wengi ambao wapo hai leo ambao wamepitia hili, na wale wanaowazunguka wanaweza kuthibitisha kuwa kweli. Kuwa tu anajiita muumini, au kuwa mshirika wa kanisa, dini au kikundi cha kidini hakutatatua matatizo yako. Lakini kutembea katika roho hutatua migogoro yako ya ndani pamoja na migogoro na watu wengine. Huwezi kupata maisha bora!

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii awali ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org/ na imechuliwa na kupewa ruhusa kutumika kwenye tovuti hii.