Nafsi na roho: tofauti ni nini?

Nafsi na roho: tofauti ni nini?

Mungu amempa kila mtu nafsi na roho. Je! kuna tofauti gani gani ya vitu hivi viwili?

12/9/20185 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Nafsi na roho: tofauti ni nini?

8 dak

“Maana neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga wawote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo”.  Waebrenia 4:12.

Kuna tofauti gani kati ya nafsi na roho?

Adamu aliumbwa kutokana na mavumbi ya dunia na akawa nafsi hai. Hisia zetu na tunavyoshuhudia vitu tunavyoviona na kusikia, vyote hujikita kwenye nafsi na hivyo huzingatia mambo ya dunia. Mambo yote ya dunia hayako imara na yanaweza kubadilika na ndio maana hisia zetu zinaweza kupanda na kushuka na kubadilika kutokana na kile kinachotokea kati yetu. Hii ndio maana pia watu ambao huiruhusu nafsi yao iongoze maisha yao hawana pumziko.

Kupitia kile ninachoona na kusikia n.k. nina mawasiliano na watu, na hii imekua na athari katika nafsi yangu, na katika hisia zangu. Mtu anayeishi kwa kufuata nafsi yake mara zote huwa hana pumziko kwa sababu ya kile ambacho watu wengine huzungumza kumhusu.

Kupitia roho yangu naweza kuwa na mawasiliano na Mungu. Lakini kama mimi ni mbinafsi, ninaishi kwa kufuata uelewa wangu, na kufuata hisia zangu ambazo ni za dunia. Ndipo mwili wangu unatumika kuutumikia ulimwengu huu, na roho pia imejazwa na kile kilicho cha ulimwengu na nina mawasiliano kidogo au sina mawasiliano kabisa na Mungu.

Lakini ukombozi wa kristo utabadilisha kabisa hili, ili niweze kuwa na mawasiliano na Mungu na kuwa wa kiroho na kimbingu badala ya kuwa mbinafsi na wa kidunia. Matokeo yake ni maisha ya uaminifu, uaminifu kwa Mungu na kwa neno lake, badala ya kuishi kwa kufuata uelewa wa kibinadamu.

Roho yetu inapaswa kufanywa kuwa hai ili Mungu aweze kuzungumza na sisi; tunapaswa tuishi kwa ajili yake na kwa mambo ya mbinguni. Ndipo tutakapopata pumziko la nafsi zetu. Mambo ya mbinguni ni ya milele na hayawezi kubadilika.tunapoishi kwa kumtukuza Mungu, tunakuwa huru kutoka kwenye kutopumzika ambako hutokana na woga juu ya namna ambayo watu watazungumza kutuhusu.

Neno la Mungu: Upanga ukatao kuwili

Hapa ndipo tunapohitaji neno la Mungu. Lina makali kuliko upanga ukatao kuwili. Huka katikati ya nafsi na roho na kutuonesha mawazo yetu yaliyojificha na matamanio yetu.

Mara nyingi huwa tunahukumu hali kulingana na hisia zetu na sababu za kibinadamu; lakini kama tukianza nitaanza kumtafuta Mungu, najiweka wazi katika neno la Mungu. Neno la Mungu hunionesha fikra za moyo wangu na hukata na kugawanya kati ya kati ya nafsi na roho – kati ya mambo ya kidunia na mambo ya kibinadamu ambayo huyapokea katika nafsi yangu, na mambo ya kiroho na kimbingu ambayo roho yangu hupokea. Napaswa kuamini neno la Mungu na kuwa mtiifu kwalo, na ndipo nafsi yangu huja katika pumziko. (Isaya 53:12)

Kwa mfano, “Shinda uovu kwa wema” Huenda moja kwa moja kinyume na hisia zetu za kibinadamau na uelewa wetu wa kibinadamu au kile tunachohisi ni kuwa ni haki; lakini kama tunaamini neno na kuwa watii kwalo, tunakuja katika pumziko. Ndipo tutakapoiona hekima ya Mungu kuwa ni kuu kuliko uelewa wetu unavyotueleza na kutuambia.

Kuna neno pia linahusu kumsamehe mtu aliyekukosea saba mara sabini kila siku. Kama wewe ni mbinafsi, utang’ang’ania yale ya dunia, na kiburi chako na uelewa wako wa kibinadamu utapanga mipango ya kulipa kisasi kwa mtu aliekukosea na utauliza wana familia na marafiki wanachofikiria n.k.

Heri uliache neno la Mungu lije na kutenganisha kati ya kile unachokielewa kupitia nafsi yako (hasa hasa kupitia hisia zako) na hekima itokayo juu, ambayo unaielewa kupitia roho yako, kupitia kile ambacho neno la Mungu hukuambia. Ishi kwa imani katika neno la Mungu na si kwa kufuata uelewa wako wa kibinadamu; ndipo nafsi yako itapata pumziko.

Ruhusu fikra zako ziongozwe na roho

Petro alimpenda Yesu, lakini alikuwa akitazama mambo kwa mtazamo wa binadamu, ambao ni kujiepusha mweyewe. Shetani ana nafasi ya kufika kwenye nafsi ya kidunia na matokeo yake ni kutokuwa na pumziko. Yesu alisema, “Ondoka kwangu, shetani!” Yesu alijua mawazo ya Mungu kwamba si kujikweza mweyewe. Sasa anataka kufanya roho zetu ziwe hai ili tuweze kupokea hekima ambayo inatoka juu ambayo ni mwanzo wa yote mazuri, n.n. (Yakobo 3:17-18)

Matokeo yake ni maisha yenye Imani ambapo tunashikilia neno la Mungu dhidi ya uelewa wetu wenyewe wa kibinadamu na hisia zetu, na utumia miili yetu kumtumikia Mungu. Ndipo nafsi zetu, ambazo ni za kidunia na zisizo na utulivu, zinakuja katika pumziko katika Mungu na fikra zetu zitaongozwa na kile roho inachosema.

“Angalieni msimkatae yeye anenaye, maana auaikiwa hakuwaokoa wale waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya nchi! Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na nem, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza pamoja na unyenyekevu na kicho;i”. Waebrania 12:25, 28

Hali yote ya kutokuwa na utulivu, manung’uniko, na hofu hutoka kwa mtu mbinafsi ambae hutaka kufanya mapenzi yake katika dunia hii. Mtu wa kiroho huishi kwa Imani katika neno la Mungu, mambo yote hufanyika kwake kwa wema. (Warumi 8:28) huyaacha mapenzi yake kila siku na hutulia kwa Mungu. Ni maisha ya utukufu na amani haya – ufalme usioweza kutikiswa.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye Makala ya Siguurd Bratlie ambayo awali ilionekana kwa kichwa cha Habari “Huchoma na kugawanya nafsi na roho” kwenye jarida la mara kwa mara la BCC “skjulte skatter” (Hazina zilizofichika) Agost 1955. Imetafsiriwa kutoka kwenye Kinorwe na imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika katika tovuti hii