“Tuonane baadaye!” Nilisema kwa furaha nilipolkuwa nikipunga mkono kutoka mbele ya mlango. Niliingia ndani taratibu, na kufunga mlango. Lakini nilijihisi mwenye hatia! Ni binti mzuri, lakini sipendi kuwa karibu naye – sijui ni kwa nini.
“Wewe ni mnafiki!” sauti ndogo ilinijia kichwani mwangu. “Unajiita mkirsto? Wakristo wanapaswa kuwapenda maadui wao; kila mmoja analijua hili. Lakini wewe hutaki hata kuwapenda rafiki zako!”
Kujaribu kupenda haikusaidia
“Nimejaribu” kujisemea kwa sauti. Ni kweli – nimejaribu. Kwa kipindi kirefu nimejaribu kufanya juhudi kuwapenda watu wanaonizunguka, hususani wale ambao sipo nao vizuri. Sijaacha kuwa karibu nao, na wanapofanya ama kusema mambo yanayonifanya nihisi uchungu, najihisi mwenye uchungu au kukereka, nimeona kwamba kero zinatoka ndani yangu, na nimekataa fikra hizi.
Lakini haijanisaidia. Kweli – lakini ni kweli siwapendi, lakini hata niliposhindwa kukata tamaa na niliamua kutokuwa na uchungu wala kukereka, kilichobaki ni utupu ndani yangu, sihisi chochote dhidi yao. Siwezi sema kwamba nilifurahia kuwa karibu yako, na sihisi kama nawapenda.
Yesu anawezaje kutulazimisha kupenda?
Kwa nini inapaswa kuwa vigumu? Wakati mwingine tena natazama juu neno linalojulikana kutoka kwenye mahubiri ya Yesu kwenye mlima ambapo anatuambia tuwapende maadui zetu.
“Lakini mimi nawambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi” Mathayo 5:44
Nilipotazama kifungu hiki, niligundua kwamba Yesu hutuambia tufanye mambo manne hapa, na mambo matatu ya mwisho unaweza kutoka nje na kuyafanya. Namaanisha inaweza kuwa vigumu, lakini kama mtu anakulaani unaweza kuwabariki. Inawezekana – huwezi sema haiwezekani! Sawa na mawili yanayofuata, unaweza watendea mema wale wanaokuchukia, na unaweza kuwaombea watu hata kama wewe ni mbaya kwao.
Lakini Yesu anawezaje kutulazimisha kuwapenda watu? Namaanisha, upendo ni hisia. Unawezaje kujifanya kuwa mtu mwingine? Unawapenda ama huwapendi? – hivi ndivyo huonekana kwangu.
Upendo ni matendo.
Baada ya muda niliamua kuzungumza na mkristo mkongwe niliyemheshimu na kumwamini sana. Nilimwambia matatizo yangu, na alimalizia kwa kusema kwamba inaonekana siyo sawa kwa Yesu kutuambia tufanye mambo ambayo hatuwezi kuyatawala, kama tunavyopaswa kujihisi dhidi ya wengine.
“Hapana, hapana, siyo kweli!” alisema. “Upendo ambao Yesu anauzungumzia siyo hisia. Ni vitendo kama mambo yote mengine anayotuambia tufanye.”
“Kweli?” Niliuliza, hapana sikuelewa alichokuwa anamanisha. “ni kweli”, alijibu. “unajua nini kimeandikwa katika 1Wakorintho 13, hujui? Hiyo ni sura ambayo mtume Paulo alieleza upendo wa Miungu. Isome kwa makini – kuna kitu kimeandikwa kuhusu hisia hapo.”
Nilifungua Biblia yangu na kuangalia. Kweli vya kutosha, katika 1Wakorintho 13:4 imeandikwa, “Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautabakari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu………
“tazama hii ndiyo maana ya kumpenda mwingine,” alieleza. “ukiwa mkarimu kwa watu, na kuwa mwema kwao, na hauna wivu dhidi yao, na hauna jeuri kwao, hivyo unawapenda, na haijalishi hisia zako zinavyokupeleka. Hivyo unatii amri za Yesu kabisa.”
Ilikuwa kama taa imewashwa kichwani kwangu! Hiki ndicho kitu naweza kufanya! Muda wote huu nimekuwa nikisubiri hisia zangu kuja kama uthibisho kwamba nawapenda watu. Nataka kuhisi kwamba nawapenda watu kabla sijaenda katika njia njia zangu za ukarimu, uvumilivu n.k. lakini ni kwa namna nyingine! Ni kile ninachofanya kwa kuwa nataka kuwapenda watu huo ni uthibitisho kwamba ni kweli nawapenda.
Ninamshukuru kwa tabasamu angavu, na kuishi na tumaini jipya ndani yangu. Sasa najua haijalishi nahisi vipi, naweza kumpenda kila mmoja ninayemfahamu kwa njia sawa na ile Yesu alivyofanya.
“Huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote, upendo haupungui neno wakati wo wote….” 1Wakorintho 13:7-8