Wasiwasi na kutoamini: Ambapo mkuu wa giza anatawala
Hata shaka kidogo kuhusu uongozi kamili wa Mungu katika maisha yako inaruhusu giza la kutoamini kuingia. Mkuu wa giza hutawala katika giza hili na hataki maisha mazuri kwa raia wake. Haichukui muda mrefu kabla ya giza la shaka na kutoamini inakuwa giza la kukata tamaa, na kusababisha mzunguko wa giza na uovu katika maisha yako ya mawazo.
Unapaswa ulichukulie kwa uzito sana ikiwa unaona kwamba roho ya kukata tamaa inataka kuingia ndani yako, kwa sababu Mungu hajatupa roho hii. (2 Timotheo 1:7.) Roho hii itakufanya ushindwe kumtumikia Mungu.
Hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tunasoma katika Yakobo 3:17. Ni safi kutoka kwa giza la kutoamini na shaka. Wakati Sauli alipoanza kuwa na shaka na mwongozo kamili wa Mungu katika maisha yake mwenyewe na ya Daudi, roho mbaya iliingia ndani yake. Alifanya jambo la kijinga zaidi katika giza hili la kishetani na kwa sababu hiyo ukuu wake na furaha yake vilimwacha milele, na hakustahili kuwa mfalme tena.
Kutilia shaka mwongozo kamili wa Mungu katika maisha yao wenyewe, na katika maisha ya wengine, kumesababisha watu wengi kuwa na wivu na imesababisha mauaji na kila aina ya taabu. Inasababisha kinyongo, wasiwasi, migogoro na machafuko. Hautakuwa na amani, wala pumziko, ukiwa na shaka na kutoamini.
Imani: Jua la Mungu
Cheche ndogo ya imani hufungua moyo kwenye jua la Mungu, na giza linapaswa kucha njia kwa ajili ya nuru. Imani katika mwongozo kamili wa Mungu hutuongoza katika pumziko, amani, na furaha. Inakuwa rahisi kuacha kila kiitu kwake Yeye anayehukumu kwa haki, na tunaokolewa kutoka kwenye mateso mengi na mabaya mengi.
Kama Sauli angeelewa maana ya kuacha kila kitu kwake yeye ahukumuye kwa haki, angeweza kuwa na furaha kweli Daudi alipoheshimiwa zaidi kuliko yeye baada ya ushindi katika vita dhidi ya Wafilisti. (1 Samweli 18:7.) Angekuwa mfalme, na angekuwa na ushirika wa utukufu, wenye matunda pamoja na Daudi. Sauli angeweza kumsifu Bwana na kufurahi pamoja na Daudi, na angeweza kuwa na utukufu mwingi kutoka katika maisha yake. Lakini mkuu wa giza, ambaye amekuja kuua, kuiba, na kuharibu (Yohana 10:10), aliweza kuharibu maisha yake yote.
Hakuna kitu kilicho katika giza kinachoweza kuishinda nuru. Ni ajabu kuwa huru milele kutoka kwenye nguvu za kutisha za giza na mzunguko mbaya wa maisha ya mawazo ya giza. Sasa mawazo yetu yanaweza kuwa juu ya kila kitu ambacho ni kizuri. Ibrahimu alimwamini Mungu, na kwa sababu aliamini, baraka zilizokuja juu yake zilikuwa nyingi kama nyota za mbinguni na mchanga wa bahari. (Waebrania 11:12.)
Haiwezekani kumpendeza Mungu bila imani (Waebrania 11: 6), lakini ikiwa tunaamini na kumtii, tunampendeza sana basi baraka zake hazina mwisho; Ni zaidi ya unavyoweza kufikiria kwa uelewa wako wa asili.
Yesu anakuja hivi karibuni kupokea utukufu na sifa kutoka kwa wote walioamini na kutii injili Yake. (2 Wathesalonike 1:8-10.) Atashiriki urithi wake pamoja nao.
" Mungu, njia yake ni kamilifu," asema Daudi katika Zaburi 18:30. Hebu tuamini hivyo!
" Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema..." Warumi 8:28. Hebu tuamini hivyo!
ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo." 1 Wakorintho 10:13. Hebu tuamini kwa kweli na tufurahie juu yake!