Hapa ndipo nilipopata uhuru kutoka katika hofu.

Hapa ndipo nilipopata uhuru kutoka katika hofu.

Niligundua kwamba hofu, japo ilikua kweli kwangu, haikutoka kwa Mungu. Na ndipo aliponionesha namna ya kuishinda.

19/5/20205 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Hapa ndipo nilipopata uhuru kutoka katika hofu.

Hofu imekua adui wangu mkubwa. Kwenye maisha yangu, nilikua nikifikiria mambo mabaya ambayo yangenitokea.

“Nilikuwa mtumwa wa hofu”

Nilipokuwa na umri wa miaka 13, nilipelekwa hospitali kufanyiwa upasuaji ghafla. Daktarin aliona uvimbe kwenye fuvu langu ambao ulikua ukijipenyeza kwenye ubongo wangu. Umekuwepo hapo kwenye maisha yangu yote na waliniambia kuwa ni muujiza kwamba sikuwa na tatizo la ubongo na kwamba sikuweza kupooza nikiwa  mtoto mdogo. Upasuaji ulifanyika kwa mafanikio na niliendelea kwenye Maisha ya kawaida ya mtu mwenye umri wa miaka chini ya ishirini, baada ya kupona. Lakini baada ya muda, nilianza kufikiria kwamba mujiza wangu ungeisha ndani ya muda mfupi, na hivyo sikua na kitu cha kutazamia mbeleni.

Kufikiria huku kusiko na matumaini kulipelekea hofu nyingine – hofu ya kupoteza kazi yangu, hofu ya kutokua na pesa za kutosha, hofu ya kupata ajali ya gari, na hofu kuhusiana na familia na marafiki zangu. Kila jambo nililodhani kwamba siwezi kulimudu lilinipa msongo mkubwa wa mawazo. Kwa miaka mingi hofu hizi hata kama zilikua za kijinga ama ilikua ni vigumu kutokea, zilikua za kweli kwangu. Mara nyingi zillikua na nguvu sana na zilitawala fikira na matendo yangu.

Baada ya muda, niligundua kwamba hofu hizi zilikua zikinitawala sana na zilikua zinanifanya nikose furaha. Nilipoanza kufikiria kuhusu sababu kwa nini nilifanya mambo fulani kwenye hali fulani, niligundua ni mara ngapi hofu yangu ilinifanya niseme ama kufanya mambo ambayo yaliwaumiza watu. Nilihisi kama mtumwa wa hofu, na nilikua na shauku ya kuwa huru!

Hofu ni roho

Katika Biblia inasema, “Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu nay a upendo na ya moyo wa kiasi.” 2Timotheo 1:7. Nilisoma kifungu hiki na niliamua kwamba ningeweza kuamini kama ilivyokuwa imeandikwa. Hofu ile japo ilikuwa kweli kwangu, haikutoka kwa Mungu. Nitambua kwamba hofu ni roho – ni “adui” ambaye siyo sehemu yangu lakini ni kitu ambacho naweza kupigana nacho. ( Waefeso 6:12) roho ambayo Mungu amenipa ina nguvu – nguvu ya kushinda roho ya hofu, hivyo inaweza kubadilishwa kwa upendo, shukrani na tumaini. Niliamua kwamba nisingeweza kamwe kuiacha iyatawale maisha yangu.

Kwa uamzi huu, nilipigana dhidi ya fikra hizi. Niliyakagua mawazo yangu katika kila hali, nilitazama kuona kama kilikua na hofu yoyote, na nilimwomba Mungu kwamba angenipa roho ya nguvu, upendo, na fikra thabiti. Kwa wakati fulani, nilichukua kila eneo husika la hofu na kulifanyia kazi. Kila wakati fikra hizo zilipokuja, nilmwomba Mungu anisaidie kuzishinda.

Sasa, naweza kusema kwamba nimeishinda hofu kwa kiasi kikubwa! Ninauwezo Zaidi wa kuiona hofu inapokuja, na ninaweza kuomba haraka na kumwomba Mungu anisaidie kushinda. Hofu hapo zamani nilihisi ni jitu kubwa ambalo isingewezekana kulishinda, imekuwa adui ambaye sasa ninajua namna ya kupambana nae. Bado kuna wakati mwingine nahisi hofu hii kubwa, lakini nimeshuhudia kwamba ninapomlilia Mungu, huja upande wangu na kunipa nguvu ninayohitaji kushinda.

Na nimeona miujiza mingi katika Maisha yangu. Kukosa tumaini kumebadilishwa na “fikra zenye tumaini la baadae” ambayo ni mawazo ya Mungu juu yangu. (Yeremia 29:11) Nimejifunza kuyaweka Maisha yangu mikononi mwake moja kwa moja na kuamini kwamba hutuma kila kitu kwa mema juu yangu.

Vifungu ambavyo vilikua silaha kwangu

Neno la Mungu lina kile ninachohitaji kabisa, na pia hapo napata “silaha” ya kushinda nilipokuwa najaribiwa kukubali mawazo haya ya hofu. Hii hapa orodha ya vifungu ambavyo vilinisaidia binafsi: “Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu nay a upendo na ya moyo wa kiasi.” 2Timotheo 1:7.

“Maana nayaju mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza. Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote” Yeremia 29:11-13.

“Katika hili pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo.” 1Yohana 4:18.

“Msijisumbue kwa neon lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.” Wafilipi 4:6.

“Akaniokoa na adui yangu mwenye nguvu, na wale walionichukia, maana walikua na nguvu kuliko mimi. Walinikabili siku ya msiba wangu, lakini BWANA alikuwa tegemeo langu. Akanitoa akanipeleka panapo nafasi, aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami.” Zaburi 18:17-19.

“Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza; Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu.” Zaburi 91:15-16.

“Yeye, siku za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu.” Waebrania 5:7.

“Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu.” Waebrania 10:35.

Chapisho hili linapatikana katika

: Makala hii imejikita kwenye Makala ya Heather Crawford awali ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org/ imechukuliwa na kupewa ruhusa hutumika katika tovuti hii.