Ibrahimu: Kuchagua kuamini katika hali ngumu sana

Ibrahimu: Kuchagua kuamini katika hali ngumu sana

Imani ya Ibrahimu kwa Mungu ilijaribiwa kwa njia ambayo wengi wetu hatutapata kamwe.

31/1/20255 dk

Written by Julia Albig

Ibrahimu: Kuchagua kuamini katika hali ngumu sana

Ibrahimu tayari alikuwa mzee Mungu alipomuahidi: " Tazama sasa mbinguni, kazihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako!" Mwanzo 15:5. Ibrahimu na mkewe Sara hawakuwa na watoto na tayari walikuwa wazee sana kupata watoto. Lakini Ibrahimu aliamini ahadi ya Mungu, hata kama ilikuwa kawaida kusema haiwezekani.

Imani ya Ibrahimu katika Mungu ilijaribiwa na ahadi hii, ili kuona kama angeamini kile Mungu alichosema bila kujali hoja yake ilimwambia nini. Ibrahimu alisimama imara katika imani yake, na Mungu alitimiza ahadi yake (Warumi 4:20). Sara akazaa mtoto wa kiume, nao wakamwita jina la mwana wao Isaka, kama Mungu alivyowaambia wafanye.

Soma zaidi kuhusu imani ya Sara hapa: Sarah: Aliamini kwamba Mungu atatimiza ahadi yake[GS1] [IH2] 

Mtihani wa pili

Lakini Mungu angejaribu imani ya Ibrahimu mara ya pili, na huu ulikuwa mtihani tofauti na mwingine wowote.

Miaka michache baadaye, Isaka alipokuwa kijana, Mungu alikuja tena kuzungumza na Ibrahimu. Mungu akasema, " Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia." Mwanzo 22:2.

Ibrahimu alipaswa kuwaza nini juu ya jambo hilo? Haikuwa na maana. Mungu alionekana kwenda kinyume na kile alichoahidi mwenyewe.

Lakini imani ya Abrahamu kwa Mungu haikuwa dhaifu. Ingawa hali ilionekana kuwa haiwezekani kabisa, aliamka asubuhi, akamwandaa punda wake, akachukua kuni ambazo zilihitajika kwa ajili ya sadaka, na kuanza safari ya siku tatu kuelekea milimani na Isaka. (Mwanzo 22.)

Tunaweza kufikiria angejaribiwa na mawazo ya shaka wakati alipopanda Mlima Moria. Mawazo kama: "Moyo wa Sara labda utavunjika, na hatanisamehe kamwe. Nitakuwa muuaji. Lazima nilikuwa nimeelewa vibaya; Mungu mwenye upendo hangeweza kamwe kutoa amri kama hiyo!"

Lakini Ibrahimu hakusikia vibaya; alitii kwa sababu Mungu alikuwa amesema, nasi tunajua yaliyotokea. Mawazo haya ya shaka ambayo Shetani alinong'oneza sikioni mwake yalishindwa na imani yake. Aliamini bila shaka kwamba Mungu angetimiza ahadi Yake - hata kama hiyo ilimaanisha kwamba angemfufua Isaka kutoka kwa wafu. (Waebrania 11:17-19.)

Imani inatupa nguvu ya kutenda

Kwa kweli, Mungu alitimiza ahadi yake. Wakati wa mwisho, alimzuia Ibrahimu kumuua Isaka, na baadaye, Isaka akawa baba wa taifa la Israeli.

Kwa njia hiyo hiyo, tunaweza kujaribiwa kuwa na shaka Mungu anapofanya kazi ndani yetu kufanya jambo na tunapaswa kuenenda kwa imani. Labda hatujui jinsi siku zijazo zitakavyoenda ikiwa tutafanya hivyo, lakini imani inatupa nguvu ya kutenda, ingawa hatuwezi kuona matokeo yatakuwa nini. (Waebrania 11:1).) Tunapokuwa na ngao ya imani, sisi pia tunaweza kupinga mawazo ya shaka ambayo Shetani anajaribu kupanda. (Waefeso 6:16.)

Mungu wa Ibrahimu ni Mungu yule yule ambaye tunamtumikia leo. Yeye ni kutoka milele hadi milele, na hakuna kitu ambacho hawezi kufanya. Haijalishi jinsi hali zisizowezekana zinavyoonekana, na jinsi nilivyo na kiburi na ubinafsi na hasira kwa urahisi kwa asili, Mungu anaweza kufanya muujiza katika maisha yangu.

Ameahidi kwamba Mimi - ambaye nina asili ya dhambi ya kibinadamu, na nimejaa kiburi na ubinafsi, na kila aina ya tamaa zingine za dhambi - ninaweza kubadilishwa kuwa kama Kristo. (Waruma 8:29)) Hata mtu mwenye asili kama yangu, na tabia zangu zote za dhambi, anaweza kushiriki katika asili ya kimungu! (2 Petro 1:4.) Ninapoamini hili na kutenda juu yake, basi nitakuwa mtoto wa Mungu na nitarithi vitu vyote pamoja na Yesu! (Waroma 8:16-17)Je, kuna sababu ya kuwa na shaka? Hapana, hata mara moja!

" Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu." Ufunuo 21:7.

Hakuna mipaka!

Tunajifunza kutoka kwa Ibrahimu kwamba imani katika Mungu inamaanisha tunapaswa kufanya jambo. Tunasoma katika Warumi 16:20: " Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi." Imani ni nini basi? Je, ni kukaa nyuma na kusema, "Ndiyo, naamini Mungu atamseta shetani chini ya miguu yangu" na kisha kusubiri hilo litokee?

Hapana, ni kwenda kwa vitendo, na kwenda kwa imani  Mungu anapofanya kazi ndani yangu kufanya jambo, kama vile Ibrahimu alivyofanya alipojaza kuni ambazo zilihitajika kumtoa mwanawe dhabihu. Inamaanisha kwamba lazima nitoe dhabihu vitu, lazima niache mapenzi yangu mwenyewe ili kufanya mapenzi ya Mungu. Kuacha mapenzi yangu ya ubinafsi ni sharti la kupokea ahadi ambayo tunaweza kushiriki katika asili Yake ya kiungu.

Hebu tufuate mfano wa Ibrahimu, ambaye utii wake  ulimfanya kuwa "baba wa imani yetu". (Warumi 4.) Amini katika ahadi za Mungu na uwe mwepesi kutimiza masharti ili Mungu akubariki! Usiruhusu imani yako na imani yako kwa Mungu kutegemea kile mawazo yako yanachokuambia. Haijalishi asili na hali yako ni nini Mungu anaweza kukuokoa na kukubadilisha kabisa! Yeye haulizi kama tunaweza, Yeye anauliza tu kama tuko tayari. Ikiwa jibu la hilo ni Ndiyo, tunaweza kufanya kila kitu kwa imani katika Yeye.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii inategemea makala ya Julia Albig iliyochapishwa awali kwenye https://activechristianity.org/ na imebadilishwa kwa ruhusa ya matumizi kwenye tovuti hii.