Inamaanisha nini kuwa na neema?

Inamaanisha nini kuwa na neema?

Dhumuni la zawadi ya neema ya Yesu ni nini? Je, neema ni kitu ninachopokea kuficha dhambi zangu, au inamaanisha kitu tofauti sana?

2/7/20254 dk

Written by ActiveChristianity

Inamaanisha nini kuwa na neema?

Mengi yameandikwa na kusemwa juu ya neema, lakini inamaanisha nini kuwa na neema?

Neema inamaanisha msamaha

Awali ya yote, neema inamaanisha msamaha. Ni zawadi ya ajabu ambayo tunapokea tunapotubu na kuziacha   dhambi zetu na kumkubali Yesu kama Mwokozi wetu. Bila zawadi hii ya msamaha, tungepotea milele. Yesu alilipia dhambi zetu, mara moja na kwa wote. (Waefeso 1:7.)

"Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana; apate kumtuma Kristo Yesu mliyewekewa tangu zamani;." Matendo ya Mitume 3: 19-20.

Neema inamaanisha msaada

Katika agano la kale, watu pia walipokea msamaha wa dhambi, kwa kutoa dhabihu za wanyama, lakini hawakuweza kupata msaada wowote wa kuacha kutenda dhambi. Ulikuwa mzunguko wa mara kwa mara wa kutenda dhambi, msamaha, kutenda dhambi na msamaha. Katika agano jipya tuna tumaini bora. Yesu alivunja mzunguko huu na kushinda katika kila jaribu. Alituwezesha pia kuja kwenye maisha ya kushinda, kwanza kwa kutusamehe dhambi zetu za zamani na kutupa mwanzo mpya, na pili kwa kutufundisha kushinda katika majaribu, kama vile yeye alivyoshinda. (Waebrania 10:20.)

"Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji." Waebrania 4:16.

"Wakati wa mahitaji." Huo ndio wakati tunapogundua kuwa tunajaribiwa kutenda dhambi. Kabla hatujaanguka katika dhambi, tunaweza kuomba msaada kutoka kwa Mwokozi wetu (ambaye pia alijaribiwa kwa njia sawa na sisi), na kupitia Roho Mtakatifu, Anatupa neema na msaada wa kushinda - kabla hatujaanguka!

Haijalishi nimefungwa katika dhambi sasa, ninaweza kupokea neema ya kutosha kushinda na kuwa huru kabisa[GS1] [IH2] .

Neema inamaanisha muda

"Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure. (Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia; tazama, wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa)." 2 Wakorintho 6: 1-2.

Tunaposoma haya na kutambua shahuku  ya kushinda dhambi, bado tuna muda wa neema juu ya maisha yetu. Lakini muda huu wa neema hautadumu milele, na hatujui bado tuna muda kiasi gani. Leo ni siku ya neema; leo tuna fursa ya kumwedea a Mungu, kupokea msaada wa kuokolewa, kuwekwa huru na kushinda, na tusiwe tena watumwa wa tamaa zetu za ubinafsi na tabia zetu za ubinafsi. Hebu tuutumie vizuri mudai wetu!

Wanyenyekevu hupokea neema

Mungu huwapa neema wanyenyekevu. (Yakobo 4: 6.) Ninahitaji kukubali kwamba siwezi kuwa mwema na safi peke yangu. Ninahitaji kukubali kwamba ninahitaji kabisa msaada wa Kristo kushinda uovu wote ndani yangu. Hapo tu, ndipo Mungu anaweza kunipa neema.

Neema pia inamaanisha kuwa kila kitu ninachofanikiwa katika ukuaji wangu wa kiroho na hata  vitu vya kidunia, nimepokea kutoka kwa Mungu, kwa hivyo ninapaswa kumpa heshima yote.

Neema inamaanisha inawezekana kuishi kwa kujidhibiti, uadilifu na kumcha Mungu

"Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;  nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;  tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema." Tito 2: 11-14.

Kwa hiyo, inamaanisha nini kuwa na neema?

Neema inamaanisha msamaha. Neema inamaanisha msaada na nguvu ya kushinda dhambi zote ambazo Mungu anatuonyesha. Neema inamaanisha muda  wa kufanyia kazi  wokovu wetu wenyewe. Neema hii inapatikana kwa wote ambao wako tayari kumkubali Yesu kama Bwana. Inapatikana kila siku, kwenye kiti cha enzi cha Mungu ambapo kuna neema, kwa wote ambao wako tayari kujinyenyekeza na kumlilia Mungu kwa ajili ya msaada na nguvu za kushinda dhambi inayoinuka ndani yao. Leo ni siku ya neema!

Makala hii ilichapishwa awali kwenye https://activechristianity.org/ na imebadilishwa kwa ruhusa ya matumizi kwenye tovuti hii

Shiriki