Andiko huua, bali Roho huhuisha

Andiko huua, bali Roho huhuisha

Hii inamaanisha nini kwangu binafsi na kwa jinsi ninavyowatendea watu wengine?

3/1/20254 dk

Written by ActiveChristianity

Andiko huua, bali Roho huhuisha

"Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu. Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.." 2 Wakorintho 3:5-6.

Andiko huua lakini Roho huhuisha - ndani yetu!

Yesu alitupatia mfano mzuri wa jambo hilo. Tunasoma katika Yohana 8:1-12 mwanamke aliyenaswa katika uzinzi na kwa mujibu wa sheria alipaswa kupigwa mawe hadi kufa. Mafarisayo walifanya hivyo kwa sababu Musa alikuwa ameamuru jambo hili katika sheria.

Lakini Yesu aliketi chini na kuandika chini. Labda alichoandika ilikuwa sheria nyingine ya Musa: "Usitamani..."Mafarisayo waliona Yesu alichoandika na wote wakaondoka, wakitanguliwa na mkubwa. Kutamani kitu ambacho ni cha mtu mwingine ni dhambi ambayo hutokea ndani ya mtu. Kwa sababu hamu hiyo ilifichwa, hakuna mtu aliyeweza kuiadhibu, na hakuna mtu aliyeweza kuitunza sheria hiyo kwa nguvu zao wenyewe. Kwa hiyo, kila mtu alihisi hatia.

Kisha Yesu akamwambia yule mwanamke, " Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena" Yohana 8:11. Kulingana na andiko la sheria, mwanamke huyo alipaswa kupigwa mawe hadi kufa. Lakini Yesu alikuja na roho ya sheria, na injili ya agano jipya, na hiyo ni kwamba tunaweza kuacha kutenda dhambi.

Yesu anasema, "usitende dhambi tena!Anatupa nguvu kwa njia ya Roho MtakatifuHivyo Tunaweza kuacha dhambi, na kwamba mwenye dhambi anaweza kuishi na kuja kwenye maisha mazuri. Hii ni bora zaidi kuliko mwenye dhambi kuuawa. Katika agano la kale watu waliogopa kuendelea kutenda dhambi, kwa sababu dhambi iliadhibiwa, wakati mwingine kwa kifo. Lakini kile Yesu alichokuja nacho kilikuwa bora zaidi. Watu sasa wanaweza kuacha dhambi na Kuja katika maisha mazuri, Maisha mapya kabisa katika Yesu Kristo.

Adiko huua, bali  Roho huhuisha - katika huduma yetu

Paulo alikuwa Mfarisayo. Alijua ni adhabu gani inapaswa kutolewa kwa kila kosa. Lakini hakujua mambo yaliyofichwa, sababu za mkosaji kufanya kile alichofanya. Kuhukumu watu kulingana na andiko la sheria inaweza kuwa na uharibifu sana linapokuja suala la kazi yetu na watu wengine. Ndiyo maana ni muhimu sana tujifunze kusikia kile Roho anachosema, kwa kuwa anajua mambo yaliyofichwa.

Paulo alikuwa katika udhaifu na hofu. Aliwaambia Wakorintho kwamba hakuja kwao na hekima ya kibinadamu, lakini kwamba ilimbidi ategemee nguvu za Roho Mtakatifu. (1 Wakorintho 2:3-5.) Kile alichoogopa ni kwamba kila kitu alichojifunza kama Mfarisayo kuhusu andiko la sheria kingemshawishi, ili asiweze kusikia kile Roho alikuwa akizungumza.

Kwa hivyo hapa alihitaji ufunuo kutoka kwa Roho Mtakatifu. Ni Roho tu ndiye angeweza kumfunulia mambo yaliyofichika. Ndiyo sababu alikuja katika udhaifu na hofu na kutetemeka sana. Hakuweza kufanya chochote mwenyewe. Kwa sababu sasa halikuwa tu suala la kujua adhabu ilikuwa nini kwa kila kosa, lakini ilibidi awaongoze watu kwenye maisha mapya.

Katika Isaya, Mungu anasema, "Nisikilizeni, watu wangu." Tunahitaji kujifunza kile ambacho Mungu anataka, mapenzi yake ni nini; tunahitaji kumsikiliza na kusikia kile anachofikiria, kwa sababu kama mbingu ziko juu kuliko dunia, ndivyo mawazo ya Mungu ni ya juu kuliko mawazo yetu. (Isaya 55:8-9.) Tunapaswa kuacha kusikiliza kila kitu cha dunia hii. Kisha tunaanza kusikia kile Mungu anafikiria juu ya mambo. Tunaanza kusikia sauti ya Roho.

Inasema zaidi katika 2 Wakorintho 3:17 , "Basi (Bwana) ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru." Hakuna uhuru wa kitu chochote tu, lakini kuna uhuru kutoka kwa dhambi, tunaweza kuwa huru kutoka kwa dhambi, na tunaweza kubadilika kuwa kama Yesu. Huu ndio uhuru ambao tunaweza kuuingia. Huu sio uhuru wa uongo, lakini ni uhuru wa kweli tunapobadilishwa kuwa kama Yesu, kutoka utukufu hadi utukufu. (2 Wakorintho 3:18.)

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imetokana na hotuba ya Kaare J. Smith mnamo Mei 28, 2019. Ilichapishwa awali katika https://activechristianity.org/ na imebadilishwa kwa ruhusa ya matumizi kwenye tovuti hii.