Jema au baya
Haijalishi Imani ipi, dini ipi au Imani gani ambayo watu wanayo, malengo yao yanafanana ni kufanya jambo lililo jema; jambo ambalo hupelekea uhuru, furaha, amani, ukuaji, na maendeleo- jambo ambalo linatufanya tuwe watu wema na kujenga uhusiano mzuri kati ya watu na mataifa.
Lakini kufanya jambo lolote jema, napaswa kwaza kujiweka huru dhidi ya mambo yote yaliyo kinyume na wema – huru dhidi ya uovu. Kama nataka kuushinda uovu katika ulimwengu huu, lazima kwanza niushinde uovu ndani yangu mwenyewe.
Chanzo cha jema au baya.
Kila jambo jema katika ulimwengu huu hutokana na chanzo chema, na kila kiovu hutokana na chanzo kiovu. “Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani ndani ya mwili wangu, halikai neno jema” Mtume Paulo anandika katika kitabu cha Warumi 7:18. Kwa hiyo injili ya kikristo inasema lazima “tusulubiwe” mwili wetu wenye ufisadi ama wenye asili ya dhambi, ambao ni chanzo cha uovu. Wagalatia (5:24)
“Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri” Mathayo 7:18. “Mtawatambua kwa matunda yao.” Mathayo 7:16. Ujumbe wa mbinguni ambao Yesu aliuleta , hubadili mti wote kutoka kuwa mwovu na kuwa mwema. Matunda mema huja kwa sababu mtu hupata maji na lishe kutoka katika chanzo kizuri. Chanzo hiki kizuri ni neno na roho mtakatifu.
Athari chanya ama hasi
“Ninyi waume, wapendeni wake zenu na msiwe na uchungu nao” anasema mtume Paulo katika kitabu cha Wakolosai 3:19. Tungejiuliza: Je, maneno yamezungumzwa kwa hasira na uchungu una athari nzuri na chanya kwenye ndoa au uhusiano mwingine wowote? Maneno machungu hufanya mambo yawe mazito na magumu; matokeo yake hakuna kitu chema, na hayaleti suluhisho kwenye tatizo lolote.
Kwa nini huwa unakuwa na uchungu na hasira? Je, si kwa sababu yako mwenyewe na hautaki kuwa huru kutoka kwenye uovu? Tamaa na mahitaji ya kwamba watu wakupendelee, au mambo yako kwa namna tofauti? Lakini kama ukiwekwa huru dhidi ya hili “Kujipenda mwenyewe” upendo wa kweli unaopata unakuwa nguvu chanya inayoyeyusha mioyo iliyoganda, kufuta machozi, kuunganisha wale waliotengana, kujenga uhusiano na uwazi, na kutoa ujasiri na kuamini! Hivyo kuwa chanya!! Fanyia kazi mambo yote yaliyo mema!!
Nguvu ya ulimi
“Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; na wale waupendao watakula matunda yake.” Mithali 18:21. Kwa ulimi wako, unaweza haribu furaha na amani na kupanda mashaka na kutoaminiana. Lakini kwa ulimi wako unaweza pia kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya kufanya kazi pamoja, kutengeneza kujenga Imani na kujiamini. Watu wote wanapaswa kula (kuishi na) tunda (matokeo) ya maneno haya.
Kisasi na Kulipiza
“Paulo anaandika katika kitabu cha Warumi 12:17 na 21, “msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote….. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.”
Kuwalipiza watu na kufanya kisasi haijawahi kuzalisha jambo lolote jema ulimwenguni. Kisasi ni mali ya Bwana. Hiyo ni kazi yake, mahala pake. Inalipa , hivyo usisfikirie kuhusu kisasi dhidi yako mwenyewe au kuwalipiza watu, bila kujali walichokifanya. Inaweza kuwa vyema kufikira kuhusu mambo uliyosamehewa, na kwamba Yesu, mwana wa Mungu ametoa uhai wake kama malipo ya dhambi zetu, na si kwa sisi peke yetu lakini pia kwa ajili ya ulimwengu wote. (1Yohana 2:2)
“Kwa ajili ya hayo nakuambia, amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa kuwa amependa sana; lakini asamehewaye, kidogo huyo hupenda kidogo.” Luka 7:47.
Huwezi timiza lolote jema kwa kutenda maovu