Je, imani yako inafaa kutetewa?

Je, imani yako inafaa kutetewa?

Unapigania nini hasa?

10/3/20164 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Je, imani yako inafaa kutetewa?

6 dak

Je, imani yako ni imani ambayo Biblia inatuambia tuipiganie?

Je, imani yako ni imani ambayo Biblia inatuambia tuipiganie?

Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu.” Yuda 1:3.

Wakati Yuda anaadika alichofanya, alikuwa hafikirii “Ukiristo wa kisasa”. Alikuwa anaandika juu ya imani waliyopewa watu watakatifu wa Mungu, mara moja na kwa wakati wote! Mara moja na kwa wakati wote, maana yake, usije baadaye ukasema kwamba Ukristo ni tofauti na imani ya awali ambayo tumepewa! Soma kilichoandikwa katika Yuda 1:17: “Bali ninyi, wapenzi, yakumbukeni maneno yaliyonenwa na zamani na mitume wa Bwana wetu Yesu kristo.”

Unapigania nini hasa?

Kwa hiyo ni imani gani hasa hii ambayo Biblia inasema tunapaswa kuipigania? Unatetea nini hasa unaposimama na kusema, “Mimi ni Mkristo?”

Kuwa “Mkristo” kunamaanisha kuwa “mfuasi wa Kristo” - kuwa na nia sawa na Yeye. Petro anaandika, “Basi kwa kuwa kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ileile, kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi.” 1 Petro 4:1. “Mwili”ni asili ya dhambi ya kibinadamu tuliyozaliwa nayo. “Kuteswa katika mwili” inamaanisha kwamba, kama Yesu, unachukua maamuzi thabiti kwamba ni vyema uteseke unapojaribiwa kutenda dhambi, badala ya kujitoa kwa jaribu hilo. Kwa kufanya hivi unaweza kabisa kuacha dhambi!

Petro anaeleza kuwa ni mateso , kwa sababu unaposema hapana kwa tamaa mbaya katika asili yako ya kibinadamu, unaenda kinyume na kile unachotaka kufanya kwa asili, na hiyo ni chungu. Lakini mateso haya yanatupeleka kwenye kitu kizuri – tunaacha kutenda dhambi, tumakuwa huru kutoka katika dhambi. Inamaanisha kufuata kufuata nyayo za Yesu kweli. Kuamini kwamba jambo hili linawezekana ndiyo imani ambayo biblia inazungumzia. Sasa hiyo ni imani yenye thamani ya kuipigania na kuitetea!

Soma zaidi: Je! Wakristo hawapaswi kumfuata Kristo?

Huwezi kutetea imani yako ikiwa unaishi katika dhambi

Maisha ya kujisalimisha kwa kile biblia inachokiita “tamaa na tamaa mbaya” ni kama kuishi kwenya gereza lenye giza. Je, unawezaje kuwaaminisha watu kwamba imani yako ndiyo imani ambayo biblia inazungumzia ikiwa bado upo katika “seli hii ya gereza”ikiwa bado unakubali dhambi? Kila mtu anaweza kuona kwa maneno yanayotoka kinywani mwako, kwa matendo yako na majibu yako, kwamba umefungwa na dhambi yako, kwamba haujaacha dhambi, kwamba hauko huru.

Wayahudi walipomwambia Yesu kwamba hawakiwahi kuwa watumwa wa mtu ye yote Yesu aliwajibu, “Amini amini nawambia, kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. Wala mtumwa hakai nyumbani siku zote; mwana hukaa siku zote. Basi mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli. Yohana 8:34-36.

Anza kuishi kama mkristo – asiye na dhambi

“Uhuru kweli” inamaanisha huru kutoka katika dhambi! Siyo bure tu kwa sababu Yesu alikusamehe dhambi zako, lakini pia uhuru wa kuamka asubuhi na kusema hapana kwa mapenzi yako mwenyewe. Huru kuchukua msalaba wako mwenyewe na kumfuata Yesuka kama inavyosema katika Luka 9:23. Huru kushinda kama alivyoshinda. Kisha maisha ni ushuhuda wa imani unayoipigania na kuitetea.

Nashukuru hatuko peke yetu. “Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, anaweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa.” Waebrania 2:18. Yesu anajua ilivyo kuwa mwenye asili ya kibinadamu kama sisi. Anajua inagharimu kiasi gani kuja kwenye maisha ya ushindi. Na ndiyo maana unapomwomba, atakusaidia kushinda mawazo na miitikio ya dhambi inayotokana na asili yako.

Kila jaribu ni fursa ya kushinda, na kila wakati unaposhinda utakuwa huru zaidi na zaidi kutoka kwa dhambi!

Ikiwa hiki ndicho unachotaka, basi usipoteze muda wo wote. Chukua biblia yako na usome mwenyewe. Mwombe Mungu akupe imani ambayo biblia inazungumzia, imani kwamba inawezekana kuwa huru kutokana na dhambi. Kisha anza kuishi kama mkristo – mkristo mwenye imani inayofaa kuipigania na kuilinda.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye makala ya E. Risa awali ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org/ imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika kwenye tovuti hii.