“Mungu ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kway eye aliufunga ulimwengu. Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa ukuu huko juu.” Waebrania 1:1-3.
Mwana pekee wa Mungu
Hivyo ndivyo alivyo mkuu, Yeye ni Mwana pekee wa Mungu. "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele." Yohana 3:16.
“Ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu.”. Wafilipi 2:6-7.
Yesu, ambaye alikuwa Mwana wa Mungu na mrithi wake wa pekee, aliacha kuwa sawa na Mungu. Alitaka kuwa na kaka na dada ambao pia walikuwa wamepata asili ya kimungu na ambao wangeweza kurithi pamoja Naye. Ilikuwa ni kutupa uwezekano huu, wokovu huu, kwamba Yesu alikuja duniani. Na alipokwisha kumaliza kazi, imeandikwa hivi kumhusu: “Hata tena amleletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, alisema, Na wamsujudu Malaika wote wa Mungu.” Waebrania 1:6
Imeandikwa zaidi kuhusu Mwana wa Mungu: “Kiti chako cha enzi, Ee Mungu, ni cha milele na milele… Umependa haki na umechukia maasi; kwa hiyo Mungu wako amekutia mafuta, mafuta ya shangwe kupita wenzio.” Waebrania 1:8-9.
Yeye ni mzaliwa wa kwanza - na inawezekana kwetu kuwa kaka na dada zake!
Tunaona kwamba ana wenzake, katika tafsiri nyingine ya Biblia imeandikwa kwamba ana ndugu, lakini ni mzaliwa wa kwanza; Yeye ndiye aliyemaliza kazi na kutupa uwezekano wa kuwa ndugu na dada zake kweli. Yesu aliona hilo kuwa jambo kuu sana kwa sababu mara tu Alipofufuka kutoka kwa wafu, Alisema: “Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ‘Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.’” Yohana 20:17.
Tunasoma jinsi alivyofurahi sana kuwa na ndugu. “Anasema, “Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu; katikati ya kanisa nitakuimbia sifa.” Waebrania 2:12. Tunaweza pia kusoma juu ya ahadi za ajabu anazowapa ndugu zake: “Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda, nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. Ufunuo 3:21.
Lakini sasa swali ni: je, tunaona ukweli kwamba sisi ni kaka na dada zake wakubwa kama vile Yeye anavyoona, ili kwamba tutaacha kila kitu ili kumpata Kristo? Yohana anaandika jambo ambalo ni la maana sana: “Tazameni jinsi Baba alivyotupenda! Upendo wake ni mkuu hata tunaitwa wana wa Mungu.” 1 Yohana 3:1.
Hili sio tu jambo ambalo tumeitwa tu, lakini ni kweli kabisa. Tunaposoma: "Yeye ashindaye ... kama mimi nilivyoshinda." Ni lazima kweli na kweli tuwe ndugu zake. "Ndiyo maana ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtabua yeye." 1 Yohana 3:1. Ikiwa tuna uthibitisho huu, tunaweza kuwa na furaha tele.