Je nina sababu yeyote ya kukata tamaa?

Je nina sababu yeyote ya kukata tamaa?

Shetani huja na mawazo ya kuvunja moyo ambayo yatakufanya usipige hatua. Je unahitaji kumsikiliza?

9/12/20155 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Je nina sababu yeyote ya kukata tamaa?

Yesu hutuambia kuishi Maisha masafi, yasiyo na lawama, na yasiyo na dhambi. (Mathayo 5:48) Lakini mara nyingi unaikuta sio rahisi kama jinsi unavyofikiri, na ndipo Shetani huja na mawazo yenye kukatisha tamaa kwamba haitofanikiwa kwako.

Ilihali upo duniani, Shetani atajaribu kwa kadri ya uwezo wake kuhakikisha kwamba hauishindi dhambi, na moja ya silaha zake kubwa kufanya haya ni kukukatisha tamaa. Hujaribu kukwambia kwamba sio rahisi kuishinda dhambi. Anaweza hata kukujaribu kukuaminisha kwamba haujaitwa! Je unahitaji kuyasikiliza haya? Hakika hapana!

Mungu hakutupa roho ya kukata tamaa

Ni rahisi kuzikubali hisia za kukata tamaa, hasa kwa sababu mawazo ya kukata tamaa mara nyingi huonekana kama ni ukweli. Kwa mfano, kwamba unadanganya. Umefanya uamuzi thabiti kuachana na kudanyanga, lakini siku moja unachagua njia rahisi nje na kudanganya ili uondokane na hali ngumu. Huenda haukusikia kengele ya mwamko asubuhi na ukaishia kuchelewa kazini, na ndipo unasema kwamba ulielewa tofauti juu ya muda ambao ulitakiwa kuanza kazi, badala ya kusema ukweli kuhusu kile kilichotokea. Baada ya yote unahisi hatia hasa kwamba haukusema ukweli, lakini ulisema uongo.

Shetani atakuja na kusema, “Angalia, umetenda dhambi. Umedanganya tena. Ni mtu wa hatari sana wewe kwamba hautokuja kuacha uongo. Hakuna tumaini tena kwako.” Anajaribu kukufanya uhisi kukosa tumaini na kukata tamaa ambapo hakuna sababu kabisa ya kuvunjika moyo. Hakika lipo tumaini kwako! Muombe Mungu msamaha na atakusamehe. Muda mwingine Mungu anaweza kukwambia uende urekebishe kile ulichodanyanya, lakini ndipo unahitaji kukiweka nyuma yako na kwenda mbele ukiwa na umakini mkubwa kuliko mwanzo kuto-kudanganya tena.

Katika hali hizi ni muhimu kukumbuka mstari katika 2 Timotheo 1:7: “Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.” Katika tafsiri ya Kinorwei imeandikwa kwamba Mungu hakutupa roho ya kukata tamaa. Kama unahisi kukata tamaa, ndipo imeandikwa hapa kwamba sio Mungu ambaye hukufanya wewe kuhisi namna hiyo. Ni kutoka kwa shetani, ambaye hukujaribu wewe kukata tamaa, na hauhitaji kumsikiliza.

Daima kumbuka kwamba Mungu hamjaribu mtu yeyote! Angeweza kuja na mawazo ya kuhukumu, kuvunja moyo ikiwa daima anahitaji kukujaza na roho wa nguvu? Anataka wewe uishinde dhambi, na daima atakupa nguvu ya kutosha kushinda ili mradi tu unaihitaji. Anakupenda sana na anahitaji tu kile ambacho ni bora kwako!



Roho ya Paulo

“Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele. Nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo.” Wafilipi 3:13-14. Ni roho gani hii Paulo aliyokuwa nayo! Hii iliandikwa na mtu ambaye alitesa na kuua Wakristo hapo mwanzo, lakini baadae alimgeukia Mungu kwa moyo wake wote.

Watu wengi wanapambana kuachana na yaliyopita. Huenda wanakaa chini na kulalamika na kulia kuhusiana na jinsi walivyo hatari na dhaifu, na kusahau kabisa kuhusu nafasi walizonazo kuishinda dhambi! Wanasahau kwamba Mungu ni mwenye kuwasamehe – na huo sio tu msamaha kidogo, ila umetimia! Usijiamini wewe mwenyewe na jinsi unavyohisi, lakini jijaze moyoni mwako kwa neno la imani kutoka kwenye neno la Mungu.

Lakini daima shinda kukata tamaa, lazima uwe na Maisha yako kwenye mpangilio. Ikiwa Mungu anakukumbusha kwamba kuna kitu fulani umekifanya, kwamba lazima ukiweke kwenye mpangilio, unahitaji kufanya hivyo. Ndipo unaweza kuinua macho yako na kuendelea, ukiamini kabisa kwamba Mungu amekusamehe.

Unajua udhaifu wako, kwa maneno mengine, kwamba kuna maeneo baadhi ambayo ni rahisi kwako kuanguka dhambini. Ikiwa utaanguka dhambini, ndipo unahitaji kuwa mwepesi kuomba kwa nguvu ya Mungu na rehema kushinda kwenye hali inayofuatia.

Na hata ikiwa unaanguka kwa sababu bado hauko imara zaidi, simama na uendelee. Kutakuwa na fursa nyingi za kujaribu tena. Usiruhusu chochote kiwe kikwazo au kikupunguzie kasi tena! Kwa wakati, utajifunza kushinda katika kila hali! “Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo Imani yetu” 1 Yohana 5:4

“Zaidi ya yote mkitwaa ngao ya Imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote ya yule mwovu” Waefeso 6:16. Amini kwamba unakwenda kuishinda dhambi! Mungu ameahidi. Anajua hakika wewe ni aina gani ya mtu na madhaifu uliyonayo, lakini amekuita! Anajua kwamba unaweza kushinda katika hali yako.

Hivyo fanya uamuzi thabiti, ndipo majaribu unayopitia yanaweza kuonekana katika njia mpya kabisa. Sio kikwazo; Ni fursa! Fursa ya kushinda!

“Piga vita vile vizuri vya Imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi.” 1 Timotheo 6:12. Kuja katika roho hiyo hiyo kama Paulo! Una Maisha mengine ya nje yakikusubiri. Na endapo bado unaanguka, hii ni kama hatua ya kupita, kwa sababu utafanikiwa! Amini katika hilo! Amini katika Mungu! Hawezi kukuacha au kukukatisha tamaa.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye Makala na Jonathan Fulglset ambayo mwanzo yalichapishwa kwenye https://activechristianity.org/ yamebadilishwa kwa ruhusa kwa matumizi kwenye tovuti hii.