“Tukamatie mbweha, wale mbweha wadogo waiharibio mizabibu, maana mizabibu yetu yachanua.” Wimbo ulio bora 2:15.
Kila kitendo huanza kwa fikra. Swali ni kwamba huwa tunafanya nini na fikra hii. Ni kama mbweha asie aonekanae kama hana hatia ambae huingia na kuharibu mizabibu, fikra za dhambi zinaweza ghafla kutoka mahali pasipojulikana na kujaribu kuharibu mioyo yetu na akili yetu. Wivu, uchungu, hasira, tuhuma – fikra kama hizi huja kwa kawaida kwetu, lakini ukweli ni kwamba ni ovu – ni dhambi. (Wagalatia 5:19-21.) Kwa hiyo tunapaswa kuwa macho na kuzikamata mara tu zinapokuja katika akili yetu, punde tu tunapoziona ndani yetu.
Nataka kutenda mema lakini……..
Lakini je, hatupaswi kuwa wakristo? Hatupaswi sote kutenda mema na kuwa na fikra safi wakati wote? Yote kwa yote tunataka kuwa wema daima, sawa?
Paulo anajibu hili kwa uwazi katika Warumi 7:18-20: “Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani ndani ya mwili wangu, haliko neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati. Kwa maana lilio jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni dhambi ikaayo ndani yangu.
Kuna kitu kinaitwa dhambi ambacho huishi ndani yetu! Hii imekaa vibaya; lakini ilikuwa vivyo hivyo kwa Yesu, alikua na dhambi iliyokuwa ikiishi katika asili yake. Alijaribiwa katika kila jambo kama sisi, lakini hakutenda dhambi. (Waebrania 4:15-16) na tunapaswa kumfuata Yesu.
Hivyo tunapojaribiwa kukasirika, kwa mfano mtu Fulani hakubaliani na sisi, tunatakiwa kuwa macho ili tulione jaribu na kukataa dhambi tuliyojaribiwa nayo. Hivyo tunamfuata Yesu. Hivyo hatui na hasira na kuchukizwa. Ndipo “tunakamata mbweha wadogo” na kuwaharibu, na mioyo na akili zetu zinabaki safi.
Tunahitaji kuwa macho
Kufanya hili tunahitaji kumwendea Mungu na kumwomba msaada kushinda fikra hizo za dhambi na majaribu. Paulo pia anatuambia katika Waefeso 4:17, “Basi nasema neno hili, tena nashuhudia katika Bwana, tangu sasa msienende kama mataifa waenendavyo, katika ubatili wa nia zao.”
Ikiwa fikra chafu inakuja, halitufanyi tuwe wachafu, ni kama tu mbweha mdogo anakuja kwenye mizabibu hapati nafasi ya kuharibu zabibu ikiwa tutamkamata kwa wakati. Lakini ikiwa tutaendelea kufikiria fikra hizo chafu, ama kujitoa kwa tamaa za dhambi, hivyo na pekee tunakua wachafu. Hivyo tunahitaji kuwa macho na kukesha ili tuweze kukamata kila fikra kabla haijapata nafasi ya kukua kuwa dhambi. (2Wakorintho 10:3-5; Waefeso 6:10-18) Kwa njia hii tunaweza kuwa baraka kwa wanaotuzunguka. "Ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu yay a kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu.” 2Wakorintho 2:14
Sifa kwa Mungu kwamba inawezekana kuishi Maisha kama haya, ili kumpendeza yeye aliyetuita na kutuchagua tangu kabla ulimwengu haujaumbwa.