Mara nyingi husemwa, "Mawazo yako yako huru," kumaanisha kwamba unaweza kufikiria kile unachotaka, kwa kuwa hakuna mtu anayeweza kusikia au kuona mawazo yako, na hakuna mtu isipokuwa wewe mwenyewe anayeweza kubadilisha mawazo yako. Lakini je, huo ndio uhuru wa kweli?
Uzoefu wangu wa kibinafsi ulikuwa kwamba mawazo yangu mengi yalikuwa mawazo ambayo sikutaka kuyafikiria. Mawazo yangu yalikuwa yakinitawala. Nilitaka kuyaondoa, lakini sikujua jinsi gani naweza kuyaondoa.
Nilimwomba Mungu anisaidie. Rafiki yangu pia aliniombea. Na muda mfupi nilipata jibu:
Nilisoma 2 Wakorintho 10:4-5 na kuelewa mistari hii kwa njia mpya, “Maana silaha za vita vyetu si vya mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome; tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo.”
Wakati fulani nilisikia ibadani kwamba mawazo yote ambayo hayaletii tumaini au imani si ya Mungu. Mawazo ya Mungu kwangu yamejaa tumaini. Kwa hiyo basi naweza kuondoa kila wazo ambalo halileti tumaini. Ninahitaji kuwa macho ili nibaki "kiongozi" kichwani mwangu. Mungu hunipa uwezo wa kufanya hivi ninapomwomba msaada.
Tangu nianze kufanya hivi, niliacha kujihisi mnyonge. Amani na furaha yangu hukua kila siku. Ninaweza kusema, kama ilivyoandikwa katika Zaburi 40:2-3, “Akanipandisha toka shimo la uharibifu, toka udongo wa utelezi; akasimamisha miguu yangu mwambani, akaziimarisha hatua zangu. Akatia wimbo mpya kinywani mwangu, ndio sifa zake Mungu wetu. Wengi wataona na kuogopa, Nao watamtumaini BWANA.