Kutoka hasira hadi baraka

Kutoka hasira hadi baraka

Rolf: Watu wengine hukasirika haraka. Mimi ni mmoja wao.

17/7/20218 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Kutoka hasira hadi baraka

12 dak

Kupata Hasira kwa haraka sana

Jambo moja lilikuwa wazi sana nilipokuwa nikikua, na hilo ni kwamba nilikua nikikasirika haraka sana.

Hasira yangu haikudumu kwa muda mrefu, na ningejihisi mjinga sana baadaye. Ilikuwa kama mlipuko mkubwa. Mara nyingi  ilikuwa ni  hasira kwa  hali fulani , sio kwa watu. Nakumbuka wakati fulani nilikuwa kazini, nikichomelea kitu, na nikakasirika sana kiasi kwamba , nikaichukua mashine ya kuchomelea na kuirusha upande wa pili  wa chumba . Sikuwahi kuumiza watu kadiri ninavyoweza kukumbuka, lakini ningekasirika sana.

Kwa kweli nilijihisi vibaya  sana kwa sababu nilijua kwamba haikuwa sawa. Nililewa  katika familia  nzuri ya Kikristo na nilimjua  Mungu. Nilitamani  kumjua kwa namna ya kibinafsi. Nilijua si  vizuri kuishi hivi, lakini sikujua jinsi ya kubadilika.

Kisha nikaoa, na nikagundua  kwamba mambo haya hayabadiliki tu yenyewe. Hakika sikuwaumiza mke wangu na mtoto wangu, au watu wengine niliokutana nao, lakini unawezaje kusaidia watu wakati uko hivyo? Nilitaka angalau kuwa na uhusiano mzuri na watu, lakini kwa sababu ya hasira yangu sikuweza kuwa na hakika kabisa juu yake.

Kuchukia maisha yako mwenyewe

Muda mfupi baada ya kuoa na kuwa baba, nilisikia injili ikielezewa kwa njia ambayo sikuwahi kusikia hapo awali. Maandiko kama 1 Petro 1:16  inasema, "  Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. hakika kilikuwa kitu ambacho Mungu alikuwa amesema, na kitu ambacho nilikuwa nimekisoma, lakini kamwe si kwa njia ambayo nilifikiri ingewezekana, kwa sababu hakuna mtu aliyejua namna ya kufanya. Lakini sasa nilisikia kwamba "Kweli, imeandikwa, kwa hiyo, lazima iwezekane." Kwa hiyo, niliposikia juu ya kuchukia maisha yako mwenyewe (asili yako ya ubinafsi, kiburi, na dhambi) na kuyapoteza, hiyo ilibadilisha kila kitu kwangu. Nakumbuka nikifikiria, "Mwishowe, sasa ninaweza kufanya kitu kuhusu mambo haya yanayonitesa!"

 

Yesu anasema: "Yeye aipendae nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele."  Yohana 12:25. Mstari huo ulifanya kazi ndani yangu. Yeye hasemi, "Yeye anayechukia wanachokiona  wengine," lakini "Yeye anayechukia maisha yake." Ni kile kilicho ndani yangu - mawazo haya yote, fikra, na vitu ambavyo vitaleta mgongano kati ya watu, ndivyo ninavyopaswa kuchukia. Kwa sababu siyo tu juu ya kuzuka kwa hasira. Nilikua nikifikiria kwamba lazima nishughulike na mambo ya nje. Lakini haipaswi tu kujishughulisha na kile watu wanachokiona, na hasira zangu. Kinachotoka  ndani yangu ndicho kinachoonyesha kile nilichokuwa nikishughulika nacho ndani.

Haikutokea yote mara moja, lakini kidogo kidogo. Nilianza kuchukia hasira vibaya sana! Nilikuwa tayari nikiichukia, lakini sasa niliichukia zaidi. Kwa sababu nilitaka kupata uhusiano na Yesu. Ikiwa nitashikilia wazo ambalo halitoshei katika ufalme wake, ninawezaje kukutana na Yesu atakaporudi? Ikiwa angeweza kurudi sasa hivi, basi nini kingetokea? Je! Mtazamo wangu ungefaa katika ufalme wake?

Kutoka kuchukia na Hasira mpaka Kubariki

Jambo kubwa ni kuchukua Neno la Mungu kama lilivyoandikwa. Mstari ambao umenisaidia sana kwa miaka mingi ni {1Petro 3:9} "… bali wenye kubariki." Nilidhani ninahitaji kuweza kubariki, kwa hiyo hiki ni kinyume (tofauti) na kile ninachofanya kwa asili. Kwa asili, mimi huleta migongano , nakosoa, nahusukuma  watu kinyume . Lakini kinyume chake, ninahitaji kubadilishwa kutoka kwenye hasira hii na kuingia  katika maisha tofauti kabisa.

Mstari mwingine ambao nilikuwa nikifikiria sana ni Wagalatia 5:24 usemao... "Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili Pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake." "Shahuku  na tamaa" ni neno la jumla kidogo. Lakini katika maisha ya kila siku, hiyo inamaanisha kuwa katika kila wazo maalum, neno, na kitendo, kwa jinsi ninavyofanya vitu, au kwa namna ninayotumia pesa yangu, nasema "hapana" kwa tamaa za dhambi katika asili yangu.

Wakati wowote ninapokuwa na mawazo juu ya kitu au mtu ambaye haendani na sheria ya Mungu, basi siwezi kubariki. Siwezi kufanya mema. Siwezi kukidhi mahitaji. Jambo la kushangaza ni kwamba nimekuwa nikipenda watu kila wakati. Nadhani labda ndio sababu ilikuwa ngumu sana, hasira hii. Sikuweza kuungana na watu na kuwaelewa, kwa sababu nilikuwa nimejaa mawazo yangu mwenyewe, na hiyo ilinitenga nao.

Asili yetu ya kibinadamu yenye dhambi, pia inayoitwa mwili, ina mambo haya tofauti ambayo mimi huyashikilia kwa urahisi, kwa hiyo nashukuru kwamba ninaweza kuyaona mawazo haya madogo, kusema 'hapana' kwayo na kuwa huru zaidi na zaidi. Pia inasema katika Waebrania 12:11 kwamba hausikii vizuri kusema 'hapana' kwa asili yako ya dhambi, lakini kwa upande mwingine, najua kwamba ninabadilishwa kila wakati. hivyo hiyo inanipa matumaini. Kidogo kidogo, ninaweza kuungana na watu na kuwa mwema kwao, bila kujali chochote. Kwa mfano, Haijalishi tena ikiwa wafanyakazi wenzangu hawakubaliani na mimi, kwa sababu ninawajali.

Kusema Samahani

Mwanzoni, pia ningewakasirikia watoto. Mara nyingi ningewaambia pole. Kwa mfano, ningesema, "Samahani kwa jinsi nilivyosema, lakini bado lazima ufanye kile nilichosema." Pengine kile nilichosema hakikuwa kibaya sana, lakini jinsi nilivyosema ilikuwa vibaya kabisa.

Baadaye, mtoto wangu wa kwanza alipokuwa mkubwa sana, nilimwambia, "Samahani sana kwa jinsi nilivyokufanyia." Nilijua haikufanywa vizuri kila wakati; kwa hasira hiyo sikuwa na ushindi wakati wote, haswa katika miaka ya mwanzo alipokuwa akikua. Lakini wanasamehe sana. Mwanangu alisema, "Baba, nakumbuka tu vitu vizuri nyumbani." Hiyo ilinifanya nilie.

Kwa hiyo tena, jinsi watu wanavyokuona kweli haimaanishi mengi sana, ikiwa unatafuta maisha ya Kristo. Unaona dhambi yako mwenyewe inayoishi ndani, na unaichukia.

Amani nyumbani

Nadhani kile kinachoelezea  nyumba yetu zaidi ni kwamba kuna amani na wema . Kwa nje huenda  haionekani hivyo. Nina watoto wa kiume wengi, na wanaweza kuwa nyumbani na marafiki wao, na wana kelele, na wakati mwingine tunabishana juu ya mambo; kuna mengi yanaendelea na ni shughuli. Lakini hiyo haimaanishi kwamba hakuna amani.

Amani ni kuwepo furaha kati ya watu, na kwamba mimi sio mvurugaji wa amani, lakini ninajenga amani. Kwa sababu tu watu wana maoni yao, na wanafanya mambo kwa njia zao wenyewe, hiyo haimaanishi kuwa hakuwezi kuwa na amani. Katikati ya hiyo panaweza kuwa na amani sana. Ninajua pia kuwa bado ninaweza kufanya mema zaidi. Ninaweza kusaidia kutengeneza  amani zaidi, kwa sababu baba ana athari kubwa juu ya jinsi patakavyo kuwa  nyumbani.. Ikiwa nina maisha ya kushinda, hiyo ina athari kubwa katika nyumba yetu.

Milipuko ya hasira huanza na wazo moja

Kile ninachojishughulisha nacho sasa ni mawazo haya madogo juu ya watu. Je! Mlipuko wa hasira unaweza kufika wapi? Baadhi ya watu huua wengine kwa sababu ya hasira, lakini vipi kuhusu fikra potofu juu ya mtu? Mara nyingi hiyo husababisha hasira. Ni ndogo sana, na iko ndani. Hakuna anayeiona. Lakini ikiwa unakubaliana na fikra hiyo na uendelee kulifikiria, je! Hiyo haiwezi kusababisha kuzuka kwa hasira?

Unaiona unapofanya kazi kwa karibu na watu. Nimeoa kwa miaka 33 sasa. Wakati mwingine ninapofikiria kidogo juu ya mke wangu, ninaona kile anachofanya au kusema, na hututenganisha. Je! Hilo siyo jambo la kuchukulia uzito? Labda siwezi kurusha vitu kwa watu au kuwapigia kelele, lakini naona bado nina mawazo haya madogo dhidi ya wengine na kile wanachofanya. Ninashukuru sana kwamba ninaweza kuona mawazo haya madogo na kuyaondoa.

Maisha ambayo hayawezi kuharibiwa

Kwa miaka mingi, nimekuwa nikifikiria juu ya kifungu kile kinachosema, “...bali kwa nguvu za uzima usio na ukomo.” Waebrania 7:15-16, Hicho ndicho kilichoandikwa kuhusu Yesu. Hayo ndio ninayotaka - maisha yaliyojaa upendo, utunzaji, wema, na furaha. Nataka kuwa mtu mwenye furaha, na furaha ambayo haiwezi kuharibiwa - hakuna kitu kinachoweza kuivunja, hakuna kitu kinachoweza kuiathiri.

Ukifikiria juu ya Yesu, ambaye alichukiwa na kukosolewa hata kabla hajaendelea na safari Yake ya mwisho, halafu wakamsulubisha msalabani, naye akining'inia hapo, lakini bado aliweza kuwaombea watu. Mara nyingi mimi hufikiria juu ya hilo. Alisema, "Baba, wasamehe, kwa maana hawajui watendalo”.  Luka 23:34.

Hivyo ndiyo ninavyotaka. Sijui maisha yangu yataishaje. Lakini maisha hayo, hakuna mtu anayeweza kuyaharibu. Hakuna kitu kinachoweza kuyamaliza. Haijalishi watu wanafanya nini, majibu yangu ya kwanza daima ni kuwa mwema kwa mtu huyo. Hayo ndiyo maisha ya Yesu na hayo ndiyo ninayoyataka - upendo, wema, haki na vitu hivi vyote ambavyo ufalme wa mbinguni umetengenezwa. Sijafika  hapo bado, lakini najua yanakuja, na ninaweza kuona maisha haya yakizidi kuwa ndani yangu ninaposhinda hasira yangu kidogo kidogo. Hiyo ndiyo injili ambayo imenigeuza.

Makala hii inategemea nakala ya Eunice Ng na Rolf van Rietschoten iliyochapishwa hapo awali kwenye https://activechristianity.org/ na imebadilishwa na ruhusa ya matumizi kwenye tovuti hii.

Shiriki