Kinyume cha furaha
Tunasoma katika 1 Petro 1: 6: "Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali."
Hapa tunaona kwamba huzuni na furaha vinaweza kuwepo kwa mtu kwa wakati mmoja. Huzuni yenyewe haihitaji kuondoa furaha.
Lakini kuna mambo mawili ambayo hayawezi kuwepo kwa mtu kwa wakati mmoja - na hayo ni furaha na dhambi. Mara tu dhambi inapoingia katika akili ya mtu na kuchukua udhibiti, furaha huondoka. Ili kupata furaha, dhambi lazima iondoke. Kwa sababu hiyo, lazima kwanza upokee msamaha, na kisha unapaswa kufanywa huru kutoka katika nguvu ambayo dhambi hii iko juu yako.
Neno la Mungu linasema hivi katika Mithali 28:13: "Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema."
Kwa hivyo kinyume cha furaha haiitwi huzuni kama watu wengi wanavyofikiria, lakini inaitwa dhambi!
Dhambi - kuishi kwa ajili yangu mwenyewe
Wakati wa kusikia neno "dhambi", watu wengi hufikiria mambo makubwa kama chuki, uongo, mauaji, wizi na uasherati. Lakini sio tu mambo haya ambayo yanaitwa dhambi katika Biblia. Biblia pia inazungumzia dhambi kama maisha ya kibinafsi (maisha yetu wenyewe au mapenzi yetu wenyewe). "Matu yeyote akitaka kunifuata," anasema Yesu katika Mathayo 16:24, "na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake,anifuate."
Katika 2 Wakorintho 5:15 imeandikwa juu ya Kristo, kwamba "Tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa aijili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliekufa akafufuka kwa ajili yao."
Hii kweli ndiyo maana ya dhambi, ni maisha na mimi katika sehemu husika. Kila kitu ni kuhusu mimi na mambo yangu, jinsi ninavyoangalia, hisia ninazofanya kwa wengine nk. Ikiwa ninafanya "tendo jema", ninashangaa ni nini wengine walio karibu nami wanafikiria juu yake.
Dhambi zote, tabia zote mbaya zina chanzo chake katika hili - maisha yangu mwenyewe. Yesu ameniweka huru kutoka katika maisha haya mazito ambapo sikuweza kuacha kuishi kwa ajili yangu mwenyewe. Sasa nina sehemu mpya katika maisha yangu - Kristo. Sasa kila kitu lazima kiwe juu Yake, mipango Yake ni nini, mambo Yake, mapenzi Yake. Katika Kristo tumeumbwa "tutende matendo mema ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuendane nayo. Waefeso 2:10. Kama ninafanya kazi hizi ambazo Mungu aliniandalia, ninapata furaha na amani ambayo hakuna mtu anayeweza kuchukua kutoka kwangu. Kazi hizi zina maana kwa maisha yangu.
Jibu kwa siri za maisha
Kadiri ninavyotakaswa kutoka kwa dhambi na maisha ya kibinafsi, ndivyo furaha yangu inavyozidi kuwa ya kina na isiyotetereka. Imeandikwa juu ya Yesu: "Umependa haki, umechukia maasi; kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amakutia mafuta, mafuta ya shangwe kupita wenzio." Waebrania 1:9. Kadiri ninavyopenda kufanya yaliyo ya haki, na kuchukia yaliyo mabaya, ndivyo furaha yangu inavyozidi kuwa isiyotetereka.
"Lakini hili lazima liwe jibu la siri ya maisha!" unaweza kusema. Hivyo ndivyo ilivyo. Fikiria kuwa na uwezo wa kuishi katika ulimwengu huu wa "uovu" na amani ya kina na isiyotetereka ambayo inanifanya niridhike kwa asilimia 100 na hali yangu maishani, na mtu mwenzangu na chochote kinachoweza kuja njiani. Si ajabu kwamba injili inaitwa Habari Njema!