Mungu anataka tuwe sisi wenyewe; Yeye mwenyewe alituumba jinsi tulivyo. Hakutaka tujilinganishe na wengine.
Watu wengi huketi na kufikiria jinsi mtu mwingine alivyo mcheshi zaidi, maarufu zaidi, wa kiroho zaidi, mchapa kazi zaidi na wa kuvutia zaidi kuliko wao na kwamba wao hawana maana. Mawazo haya huanza kidogo sana lakini hukua kwa urahisi na kuwa makubwa zaidi kadri muda unavyoenda.
Mimi mwenyewe nimepoteza masaa, siku za maisha yangu nikijilinganisha na mtu mwingine na kutamani kuwa kama wao. Nimejihangaisha mwenyewe, nimejaribu kubadilisha njia yangu ya kuishi, nimejaribu kubadilisha utu wangu ili kuwa kama mtu mwingine. Nimekuwa kwenye safari nzuri sana na marafiki zangu wema, lakini kujikuta tu nikihisi siko mwema vya kutosha na siko salama.
Kujilinganisha wenyewe na wengine inaweza kuwa uharibifu kweli ikiwa tutakubali.
Mkatae mshtaki
Mawazo haya yote yanatoka sehemu moja tu: kutoka kwa Shetani, mshtaki. Anajaribu kutufanya tuhisi kuwa hatuna maana na kuhukumiwa, na anataka kutupeleka mbali na kazi ambayo Mungu anataka kufanya ndani yetu. Ikiwa hawezi kutushtaki kwa marafiki zetu, atajaribu kutufanya tujishtaki wenyewe!
Najua mtu anayemcha Mungu aliwahi kusema kwamba ikiwa kuna machafuko, kutokuwa na uhakika na ukosefu wa usalama ndani yangu, ni ishara ya uhakika kwamba mshtaki yuko kazini. Watu ambao wanajitoa kwa roho ya mashtaka hutilia shaka kila kitu. Hakuna kitu kinachoweza kumfanya mtu kuwa tupu kama roho ya mashtaka. Ndiyo sababu lazima tuwe macho na kujilinda - kama vile ungejilinda na moto wa kuzimu - kwamba kamwe haturuhusu chochote cha roho hii ndani ya mioyo yetu.
Hatuna haja ya kumsikiliza mshtaki tena - ni vyema kiasi gani! Mungu amepanga maisha yetu yote, na anataka kila kitu kiende vizuri kwa ajili yetu. Anapanga mustakabali wa matumaini kwa ajili yetu (Yeremia 29:11), na utu na hali ambazo kila mmoja wetu anayo - sio ya mtu mwingine yeyote! Ikiwa sisi ni waaminifu kwake, basi atatutunza.
Mungu ametuumba kama tulivyo. Kila mmoja wetu ameumbwa kama mtu wa kipekee na wa ajabu. Hatuna haja ya kuwa kama mtu mwingine yeyote - tunaweza kufanya kazi na kile ambacho Mungu ametupa. Tunaweza kujifunza kutumia haiba zetu kwa wema - kila mmoja ana mchango wa kufanya kwamba hakuna mtu mwingine anayeweza!
"E e Bwana, umenichunguza na kunijua. Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu; Umelifahamu wazo langu tokea mbali... Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana,." Zaburi 139:1,2,14.