Rais wa zamani wa Marekani, Thoodore Roosevelt, alisema “Kulinganisha ni wizi wa furaha.” mara nyingi nimekuwa nikiwaza hivi, nikilinganisha na mtu mwingine, mimi niko vibaya.
“Kwa nini ni rahisi kwake kuzungumza na watu? Kila mtu anampemda. Kwa nini sipo kama vile? Natamani ningekua maarufu.”
“Mara nyingi watu huomba ushauri na msaada kwake. Na kamwe hawaniulizi mimi. Nadhani msaada wangu hauna thamani yoyote.”
“Hushughulikia Maisha vyema sana. Kwa nini daima nahisi kama nahangaika kujua nini cha kufanya?”
“Natamani… lazima iwe vizuri. ingekua rahisi… kwa nini siyo mimi...?”
Mungu anajua na hupanga mambo yote.
Mawazo haya huiba furaha moja kwa moja kutoka Maishani. Siku ambayo ilikua na jua tele ghafla inaweza kuwa giza na huzuni. Kwa nini? Kwa sababu ghafla sipo vizuri zaidi napojilinganisha na mtu mwingine. Maisha yangu si mazuri napolinganisha na ya mwingine.
Lakini Mungu hajatuumba kuwa sawa. Alimuumba kila mmoja wetu na utu wa kipekee, talanta na vipawa. Mazingira ya kipekee. Na ndiyo inanihusisha na mimi. Kukana hili, ni kusema kwamba Mungu hakujua alichokua anakifanya aliponiumba, alipopanga maisha yangu. Kama ninamwamini Mungu, hivyo ninaamini kwamba aliniumba kama nilivyo, na kwamba binafsi ananijali mimi.
“Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; chuoni mwako ziliandikwa zote pia, siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado. Mungu, fikra zako zina thamani nyingi kwangu; Jinsi ilivyo kubwa jumla yake!” Zaburii 139:16-17
Sasa ni jukumu langu kutumia kile alichonipa kuwatumikia na kuwabariki wengine. Na siwezi kufanya hivyo kwa kumtazama mwingine na kutamani ningekuwa zaidi yao.
Katika injili ya Yohana tunasoma habari jinsi Petro alivyomuuliza kuhusu Yohana. Katika kujibu Yesu alimwambia “Imekupasaje wewe? Wewe nifuate mimi” Yohana 21:20-22.
Kiukweli ni rahisi. Kuna kitu kimoja cha kujali, nacho ni kwamba namfuata Yesu. Haijalishi huyu ama yule anachofanya. Si jukumu langu, kiukweli! Lazima nimfuate Yesu. Kama nikilifanyia kazi hili kwa kweli katika Maisha yangu nitakuwa huru kutoka katika wivu na kufikiria kwamba mimi nipo chini ya wengine, huru kutoka kwenye huzuni. Na huru kutoka kwenye machafuko yanayokuja napojilinganisha na wengine.
Kazi ambayo Mungu amepanga kwa ajili yangu.
Hivyo ninachotakiwa kufanya ni kuacha kujilinganisha na watu wengine, na kuwa mwaminifu kwa uongozi wa Mungu katika maisha yangu wenyewe. Siwezi kuwa kama huyu ama yule, mtu anayeonekana kuwa “aina sahihi” ya mtu, anayeonekana kuwa na vipawa na talanta zote. Ninachoweza kufanya ni kuishi Maisha yangu kwa kufuata neno la Mungu.
Paulo anaandika “Jitunze nafsi yako, namafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia.” Timotheo 4:16. Nikizingatia kufanyia kazi maendeleo yangu mwenyewe kwa kuwa huru dhidi ya dhambi inayoishi katika asili yangu ya kibinadamu, nitakua haswa mtu ambaye Mungu alitaka niwe aliponiumba. Nitakuwa na uwezo wa kufanya kazi ambazo amezipanga kwa ajili yangu nifanye.
“Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuendane nayo.” Waefeso 2:10.
Hivyo ninapojaribiwa kujilinganisha na wengine, najua nahitaji kufanya nini. Namwomba Mungu ili anisaidie: “Ahsante, Mungu, kwamba umeniumba kama nilivyo. Nisaidie kuwa mnyenyekevu ili niweze kuona jinsi ya kumfuata Yesu katika kazi zilizopangwa kwa ajili yangu.”
Nikiendelea kuzingatia kumfuata Yesu, na siyo kutamani kwamba ningekuwa mtu Fulani, hivyo atanipa msaada ninaohitaji kuwatumikia na kuwasaidia wengine kwa kutumia kile nilichopewa, na kuwa msafi mbele yake mwenyewe.