Kutoka kwenye vinywa vya watoto wachanga - Somo katika msamaha

Kutoka kwenye vinywa vya watoto wachanga - Somo katika msamaha

Wakati tuliposhuhudia ubaya wa ubaguzi dhidi yetu, mtoto wangu wa miaka 5 alijua njia bora ya kuushughulikia.

29/6/20174 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Kutoka kwenye vinywa vya watoto wachanga - Somo katika msamaha

7 dak

"Mpendwa Mungu, tafadhali mpe kijana nafasi nyingine…"

 

Ghafla nikagundua kilichokuwa kinatokea. Niliangalia pembeni na kujiuliza ikiwa nimesikia sawa. Mtoto wangu mdogo wa miaka mitano alikuwa amepiga magoti akiomba kwa ujasiri kwa mtu ambaye alijua angemsikia. Maneno yake yalikuwa mazito sana, lakini yakiamini. Alitazama pembeni kimya kimya alipomaliza. Kisha akainuka na kusema, "Mama, ninaweza kupata aisikrimu?"

 

Bado nilikuwa nikishtuka na kupona kutokana na kile kilichokuwa kimetokea. nikihangaika kupata maana yake. Na mtoto wangu kimya kimya alikuwa ameenda

 

Tukio la kutisha

 

Yote ilitokea saa moja iliyopita baada ya mandari ya darasa la mtoto wetu mkubwa. Tulikuwa tunaelekea kwenye gari lililokuwa limeegeshwa mbali chini kwenye mtaa. Sote tulikuwa tunaangalia chini, tukijaribu kuweka kando-nyufa za barabara, wakati tuliposikia kelele kubwa ya magurudumu ya gari ikienda upande mwingine. Kila mtu aliangalia juu bila kufikiria.

 

Sote tulishtushwa na kile kilichotokea baadaye. Dereva, ambaye alionekana kama alikuwa na umri wa miaka 20, alishusha dirisha lake na kutupigia kelele kwa kututukana!  "Rudini kule mlikotoka", na kisha akatupa maneno machache zaidi kwa lugha ambayo hatukuelewa, huku akituelekeza kwa vitisho kila wakati.

 

 

Ilikuwa katikati ya mchana na hakukuwa na watu wengine barabarani na mtazamo wa haraka uliniambia kuwa hakuna msaada uliokuwa karibu. Nilisali sala ya haraka na tukakimbilia kwenye gari yetu. Nilisikia gari likiwasili tena na moyo wangu ulikuwa ukipiga kwa kasi. Sikujua ikiwa alikuwa akigeuka kurudi. Watoto walikuwa wamekasirika. "Kwa nini alikuwa akitupigia kelele, Mama?" "Alikuwa akisema nini?" "Mpigie baba!" - watoto walikuwa wakiuliza nilipokuwa najitahidi kuendesha gari kutoka kwenye eneo letu la maegesho.

 

Kuishughulikaia

 

Nini kilikua kimetokea? Nilikua naenda kuwambia nini? Ningewaelezeaje kwamba tumebaguliwa kwa sababu ya rangi yetu? Je hili litaathiri mwaka wao shuleni? Je tungehitajika kubadili shule? Vipi iwapo watapata ndoto mbaya? Vipi endapo dereva atarudi na kujaribu kuwadhuru walipokuwa wanatoka shule siku nyingine?

 

Ubaguzi wa rangi ulikuwa umeonyesha tena ubaya wake wa kutisha wakati haukutarajiwa, na sikujua nini cha kusema. Kumbukumbu za utotoni za kuonewa kwa rangi yangu ya ngozi zilirudi na zilitaka kunidhibiti. Nilipigana dhidi ya mawazo ya kutisha ambayo yalitishia kuchukua nafasi na kuomba kwa Mungu anisaidie na anipe hekima ya kujua nini cha kusema kwa wavulana wangu wawili wadogo.

 

“Kama mtu yeyote miongoni mwenu amepungukiwa na hekima na amwombe Mungu, yeye awapaye watu wote kwa ukarimu wala hana kinyongo, naye atapewa.” Yakobo 1:5

 

Tulipofika nyumbani, tulikaa na tulizungumza. Niliwaambia kwamba hawakuhitaji kuogopa mtu yeyote. Niliwaonyesha kile "mboni ya jicho letu" ilikuwa nini, na nikaelezea kuwa ikiwa mtu atawadhuru, atakuwa anadhuru jicho la Mungu.

 

“Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Baada ya yeye kuniheshimu na kunituma mimi dhidi ya mataifa yaliyokuteka nyara, kwa kuwa yeyote awagusaye ninyi, anaigusa mboni ya jicho lake.” Zekaria 2: 8.

 

Niliwaambia kamwe wasiogope kusimama na kupigana kujitetea. Niliwapa vidokezo vyote vya kujilinda ambavyo ningeweza kufikiria, ambavyo nilikuwa nimewahi kuvitumia. Niliwakumbatia karibu yangu na kwa pamoja tuliomba. Nilianza na kumshukuru Yesu kwa kutuweka salama na nikamwomba tena awalinde watoto wangu wadogo wa kiume na kuwa pamoja nao na kuwajulisha kwamba alikuwa pamoja nao kila wakati.

 

Baba, wasamehe

 

Ikaja sauti ndogo: "Mpendwa Mungu, tafadhali mpe kijana nafasi nyingine…"

 

Na hapo ndipo iliponigonga. Hiyo ndiyo ilikuwa sala sawa na ile iliyokuwa imeombewa zaidi ya miaka 2000 iliyopita.

 

"Ndipo Yesu akasema,"Baba, wasamehe, kwa maana hawajui watendalo." Luka 23:34.

 

Kwa hasira yangu ya haki, nilikuwa nimesahau kusamehe. Katika mwishi, hilo ndilo linalotakiwa katika umilele wetu. Kutenda kama Yesu. Mtoto mdogo ndiye aliyenikumbusha; litakuwa somo ambalo sitasahau kamwe - "kutoka kwenye kinywa cha watoto wachanga."

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii inategemea makala ya Roshini Sacra iliyochapishwa hapo awali kwenye https://activechristianity.org/ na imebadilishwa na ruhusa ya matumizi kwenye tovuti hii.