Je! Kwa nini Mungu huwa hazungumzi kutoka mawinguni?

Je! Kwa nini Mungu huwa hazungumzi kutoka mawinguni?

Kwa nini hafanyi iwe rahisi kwangu kuamini?

19/9/20164 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Je! Kwa nini Mungu huwa hazungumzi kutoka mawinguni?

6 dak

Watu wengi wana mawazo yenye mashaka. Sasa kwa nini Mungu hafanyi iwe rahisi kwangu kuamini? Kwa nini huwa hazungumzi kutoka mawinguni na kujionesha kwangu?

Mashaka huja kwa njia na maumbo mengi. “Je! Mungu anataka nifanye nini hasa kwenye maisha yangu”? “kwa nini huruhusu magonjwa na ajali kutokea?”na “kwa nini huhisi yuko mbali sana?”

Mbona siyo rahisi kuamini?

Mungu ni wa ajabu. Aliumba ulimwengu wote. Pia kwa upendo alimuumba kila mtu. Nguvu yake haina kikomo. Bali ni mawazo yangu ambayo hufanya iwe vigumu kumwamini Mungu. Njia ya Mungu na mawazo yake hayawezi kueleweka kirahisi kwa kutumia akili yangu ya kibinadamu.

Mungu hanichagulii, ananiacha nichague mwenyewe ikiwa nataka kumwamini au La. Hunipa uhuru wa kuchagua kumwamini na kumpenda.

Kwa kila jambo analoliruhusu Mungu litokee, anajaribu kutuleta karibu yake, pia kwenye hali inayoonekana kutokuwa na maana ama hata hali ya kusikitisha.

Mbona nahitaji kumwamini Mungu?

Mungu ana lengo mahususi na furaha ya baadae kwa kila mtu anaemwamini, haijalishi mimi ni nani au natokea wapi. Kwa kweli, Mungu amefanya iwezekane kwamba ye yote, popote, anaweza kumwamini na kumjua kwa binafsi.

Mipango ya Mungu ni mbali sana na kile ninachowaza. Kama sehemu ya mpango wake, alimtuma mwanae, Yesu, aishi duniani, na alimpa roho wake mtakatifu. Yesu alikuwa na asili kama yangu, lakini kwa kumheshimu Mungu kila wakati, kamwe hakutenda dhambi. Sasa inawezekana kwangu kupata msaada ule ule kutoka kwa roho mtakatifu kuacha kutenda dhambi. Kwa kumwamini Mungu na kumtii roho wake, naweza kuwekwa huru kutoka kwenye mzigo mzito wa kushindwa kuacha kutenda dhambi, kutokwa kwenye “kutenda dhambi na kuomba msamaha” zaidi na zaidi.

Ninahitaji roho mtakatifu wa Mungu kuamini na kuelewa ambacho Mungu, katika pendo lake amenipangia. Mungu ni rafiki ambaye hutoa nguvu kufanya yale nisiyoyaweza kwa uwezo wangu mwenyewe.

Je! Ninaamini vipi?

Kuamini ni chaguo ambalo mimi hulifanya, siyo hisia. Na napaswa kufanya jambo fulani, Hatua ya kwanza ni kumwomba Mungu msamaha nikiwa na nia ya kweli ya kuacha mambo yote nayojua kwamba ni dhambi na mabaya.

Ninahitaji roho mtakatifu wa Mungu kwa ajili ya nguvu ya kuacha kufanya dhambi. Kupokea roho wake, ninahitaji kumwomba na kusoma neno la Mungu, na kuanza kufanya mambo ninayosoma. Napaswa kutii ninachosoma kwenye biblia. Mungu huwapa roho wale wanaomtii (Matendo ya mitume 5:32)

Kuna hadithi kwenye biblia ya nabii, Eliya, aliyemwomba Mungu na kusubiri jibu. Kwanza, tetemeko la ardhi lilikuja na kisha moto, lakini Mungu hakumjibu Eliya ndani yake. Baada ya hapo Mungu aliongea kwa sauti ndogo ya utulivu. (1 Wafalme 19:12) Leo Mungu huzungumza nasi kupitia roho wake kwa utulivu uleule kama alioongea na Eliya.

Kumsikia roho wa Mungu kila siku ninahitaji kupenda kuliko ninavyopenda mitandao ya kijamii, mawazo ya rafiki zangu juu yangu, na kazi yangu. Ninahitaji kumpemda Mungu na ninataka kuwa kama yeye. Ninapaswa kupenda kile anachosema.

Ninapopokea roho wake, naanza kupokea “mawaidha” tulivu katika siku yangu. Ninakumbushwa kuhusu mambo nayoweza kuyafanya vizuri, na maombi yangu yanajibiwa.

Pengine naamka nikiwa sijisikii vizuri. Roho hunikumbusha kwamba kuwa na chuki na hasira ni dhambi. Huwa namwomba Mungu anisaidie nisiwe na chuki. Kwa msaada wa roho, ninaweza kuchagua kutokuwa na chuki hata kama nahisi hali hii.

Pengine namwombea mtu ninayemjali. Ninakutana nao siku hiyo hiyo napata nafasi ya kusema kitu kizuri kwao. Ninapokuwa na roho wake, ninapokea majibu ya maombi yangu na kumwona Mungu katika hali ya kila siku.

Wakati Mungu anapoonekana kuwa mbali, lakini muda wote yupo karibu. (Matendo 17:24-27; Zaburi 139:9-10) ninaweza kumwomba na kumwamini hata kama sijihisi kuwa na imani ya kutosha. (Zaburi 145:18)

Inawezekana nisipate majibu ya maombi yangu kwa haraka kama ninavyotaka! Maji yanayotiririka kwa muda fulani yanaweza kutengeneza jabali gumu, siyo kwa kutumia nguvu ya kulazimisha lakini kwa kutokukoma. Yesu anaweza kusaidia kabisa wanakuja kwa Mungu kupitia kwake. (Waebrania 7:25)

Mungu hazungumzi na mimi kutoka mawinguni moja kwa moja. Anataka nichague kumwamini na kwamba nifanye jambo kwa upande wangu. Ninapochagua kumwamini na kumtii Mungu ndipo mbele yangu kutakuwa na mwanga na ahadi!

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye Makala ya Anita Evangelisti awali ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org na imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika kwenye tovuti hii.