Lakini marafiki zangu watasema nini….?

Lakini marafiki zangu watasema nini….?

Je! niko huru kumtumikia Mungu au ninafungwa na mambo ambayo wengine wanaweza kufikiria kunihusu?

6/3/20173 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Lakini marafiki zangu watasema nini….?

"Naonekanaje?" "Labda niseme kitu ili nionekane mwenye  kuvutia zaidi ..." "Sipendi utani huu, lakini nitacheka ili nisiachwe nje ya mazungumzo." "Kwa hakika sitaki wengine wafikirie kuwa ninaboreka."

Si rahisi kuwa mtoto leo, na ninahisi shinikizo kubwa ikiwa kila wakati ninataka kila mtu anifikirie vyema. Ninaona kwamba yale ambayo marafiki wangu wanasema na kufikiria kunihusu ni muhimu sana kwangu, lakini vipi ikiwa hilo litanizuia kuishi jinsi Mungu anavyotaka niishi, maisha ambayo ninaweza kufanya kile hasa ambacho Mungu anataka nifanye, bila kujali watu watakavyonifikiria? 
Ninataka nini, ndani kabisa ya moyo wangu? Je, ninataka kuwa huru kabisa kutokana na mawazo hayo yote kuhusu yale ambayo wengine wanaweza kufikiria dhidi yangu?

Mungu yupo kwa ajili yangu!

Mungu hataki nifungwe na yale ambayo watu wanaweza kufikiria juu yangu. Anataka niishi maisha tofauti kabisa - maisha ambayo niko huru kufanya na kusema kile anachotaka nifanye.

“Kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuweka misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.” Waefeso 1:4.

Mungu aliniona, alinijua na kunipenda hata kabla hajaiumba dunia. Anataka niishi maisha yasiyo na dhambi. Haya ndiyo maisha pekee yanayoweza kunifanya niwe na furaha na uhuru wa kweli. Hebu fikiria kuweza kusimama bila lawama mbele za Mungu, kila siku! Ikiwa hili ndilo lengo langu, nina lengo tofauti kabisa maishani!
Mungu anapoupata moyo wangu wote, Anaweza kuangaza nuru yake pale ambapo palikuwa na giza hapo awali. Ambapo sikujua la kufanya, Anaanza kunionesha ninachopaswa kufanya ili kuwa huru kabisa na wasiwasi na hofu ya mambo ambayo watu watasema au kufanya. Neno la Mungu ni mwongozo wangu, napaswa kupima mawazo yangu ikiwa ni sawa na Neno la Mungu. Na kwa msaada wa Mungu ninaweza kukataa mawazo yote ambayo si mazuri na safi na yenye matumaini! Ndipo ninashinda!

Na Mungu huwasaidia kabisa wale ambao hutoa mioyo yao kwake. Katika Warumi 8:31, imeandikwa, “Basi tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwa upande wetu, ni nani aliye juu yetu?"

Mungu yupo kwa ajili yangu! Je, kuna sababu yoyote basi ya kuwa na wasiwasi kuhusu marafiki zangu watasema nini? Je, bado ninapaswa kufikiria kuhusu yale ambayo wengine wanaweza kufikiria kunihusu na jinsi ninavyoonekana? Hapana kabisa! Ninaweza kuinua kichwa changu na kuishi kwa ajili ya Mungu. Ana nguvu zaidi ya kutosha kunisaidia, bila kujali mimi ni nani.

Msaada wa kweli kwa marafiki zangu.

Ninapoishi kwa ajili ya Mungu, ninaweza kuwa msaada wa kweli kwa marafiki zangu, kwa sababu nina mwalimu bora zaidi ulimwenguni. Ninaporuhusu Roho aniongoze na kunionesha la kufanya, ninaweza kujifunza kufanya maamuzi mazuri na machaguo ambayo pia yatakuwa mazuri kwa wale walio karibu nami. Najua kuna kitu zaidi ya jinsi mambo yanavyoonekana kwa nje. Fikiria kwa kiasi gani hali hiyo inavyoweza kuwasaidia marafiki zangu!
Ninapomwamini Mungu aliye hai, na kufanya kile Anachosema na kile kilichoandikwa katika Biblia, ninakuwa kielelezo cha kweli. Biblia inaandika kuhusu kuwa kichwa na si mkia. Badala ya kufuata yale ambayo wengine hufanya, ninaweza kumfuata Yesu katika kila jambo ninalofanya na kufikiria. Kisha ninashika amri za Mungu, na ahadi zake zote ni zangu!

“Bwana atakufanya kuwa kichwa, wala si mkia; nawe utakuwa juu tu, wala hutakua chini; utakapoyasikiza maagizo ya Bwana, Mungu wako, nikuagizayo hivi leo, kuyaangalia na kufanya.” Kumbukumbu la torati 28:13.

Anataka niwe mwenye furaha na huru. Kwanza hapa duniani, kisha badae katika uzima wa milele.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye Makala ya Janne Epland awali ilichapishwa katika https://activechristianity.org/ imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika katika tovuti hii.