Kulikuwa na mitihani ambapo ilipaswa kusoma na kulikuwa na nguo nyingi za kufua. Nilitaka kuwapeleka wadogo zangu kufanya mahemezi na kumsaidia mmoja wa marafiki zangu ambaye alikuwa na mtoto mchanga, lakini sikuwa na muda.
Badala ya kuwa pamoja na marafiki zangu, nilikuwa nyumbani na nguo nyingi za kufua na rundo la vitabu. "Sina muda wa kufanya chochote chema," nilikuwa nikifikiria. Lakini ghafla niligundua kuwa nilikuwa nikihisi kutofurahishwa na hali yangu. Kisha mstari ukanijia: " Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu." Wakolosai 3:23.
"Je, ninaweza kufua nguo zangu kama kwa Bwana?" Nilijiuliza. "Je, ninaweza kufanya kazi yangu ya shule kama kwa Bwana?" Nilijua jibu lilikuwa "ndiyo" kwa sababu chochote unachofanya inamaanisha kila kitu unachofanya. Badala ya kulalamika na kujihurumia wakati wa kufua, ninaweza kumwombea mtu, kufikiria juu ya Neno la Mungu, au hata kuimba wimbo wa kutia moyo. Badala ya kufanya kazi yangu ya shule bila kupenda, ninaweza kuifanya kadri niwezavyo na kushukuru kwamba nina fursa ya kupata elimu.
Haya ni aina ya mambo ninayoweza kufanya kila siku ili kuonyesha upendo wangu kwa Mungu. Mambo haya "yamefichwa" katika mawazo yangu. Hayataniletea sifa au heshima yoyote kutoka kwa wengine, lakini yataleta baraka za Mungu katika maisha yangu!
Wakati wa kufua, Neno la Mungu linaweza kunijaza furaha na kunifanya niwe huru kutoka kutoridhika!
" Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;." Waefeso 6: 17-18.
Ninapomwomba Mungu anisaidie katika hali zangu, Yeye hunipa Neno lake ambalo ni silaha ya kushinda mawazo ya kulalamika. Silaha yangu ikiwa ni Neno la Mungu, ninaweza kumpenda na kumtumikia Mungu popote nilipo, na chochote ninachofanya, ninaweza kukifanya kwa moyo wangu wote kwa ajili ya Mungu!